Tangazo

June 20, 2012

NBC yatoa Dola za Kimarekani 70,000 kusaidia Tuzo za Makampuni Bora

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kushoto) akizungumza katika hafla ambyo NBC ilikabidhi hundi ya Dola za Kimarekani 70,000 kwa ajili utafiti wa kupata makampuni bora 100 ya kati unaoandaliwa na kampuni ya KPMG kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwananchi Communications. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KPMG Tanzania, David Gachewa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Dola za Kimarekani 70,000 kwa waandaaji wa utafiti wa kupata makampuni bora 100 ya kati, Mkurugenzi Mtendaji wa  kampuni ya KPMG, David Gachewa (kulia) na Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications, Theopil  Makunga. Hafla ya makabidhiano imefanyika jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (katikati) akishikana mikono na Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications, Theopil Makunga  katika hafla ambayo NBC ilikabidhi hundi ya Dola za Kimarekani 70,000 kwa ajili utafiti wa kupata makampuni bora 100 ya kati unaoandaliwa na kampuni ya KPMG kwa kushirikiana na MCL. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KPMG, David Gachewa.

No comments: