Tangazo

June 21, 2012

Vodacom kushirikiana na TanTrade katika Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam

Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda akikabidhi simu ya mkononi aina ya Blackberry na moderm kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Samuel Mvingira jijini Dar es Salaam leo, baada ya Vodacom kutangaza udhamini maalum katika sekta ya mawasiliano wakati wa Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Vodacom Tanzania itaendesha matangazo na vyombo vya habari kabla na baada ya maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 28 na kufungwa Julai 8.2012. Picha na John Badi wa Daily Mitikasi Blog

Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda (katikati), akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Samuel Mvingira na Afisa Mwandamizi wa TanTrade, Bi. Masha (kushoto), kabla ya kuanza mkutano na waandishi wa habari.

No comments: