Tangazo

June 4, 2012

Tafrija ya Wafanyakazi wa IPP yafana

Jumamosi Juni 02.2012, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi aliandaa Tafrija ya Chakula cha Usiku kwa Wafanyakazi wa Makampuni Tanzu ya IPP katika Ukumbi wa Mlimani City ambapo mambo yalikuwa safi, watu walikula kunywa na kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na Bendi ya B Band inayoongozwa na Mawanamuziki Banana Zoro. PICHANI: Mmiliki na Mhariri Mkuu wa Blogu hii, John Badi (katikati), akiwa na kiongozi wa B band Banana Zoro na Mwanamuziki nguli, Zahir Ally Zoro (kushoto). PICHA JUU: Kiongozi wa B Band, Banana Zoro (kulia) na Baba yake, Zahir Ally Zoro wakitumbuiza katika tafrija hiyo. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi akiwa katika picha ya pamoja na Waafisa Waandamizi wa kampuni tanzu za IPP wakati alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City.

Dk. Mengi akibadilishana mawazo na waafisa waandamizi wa IPP.

Mzee Dk. Mengi akiwasili ukumbini huku akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga.


Dk. Mengi akiwahutubia wafanyakazi wa IPP. Moja ya mambo makubwa yaliyoweza kuwagusa wafanyakazi hao katika speech ya Mzee Mengi ni pamoja na lile la baadhi ya kampuni tanzu za IPP kuwa listed katika Soko la Hisa jambo ilikalowawezesha staff vile vile kununua hisa nao kuwa sehemu ya wamiliki.

Dk. Mengi na Mwanae Abdiel wakiwa wenye nyuso za furaha wakati wakipigiwa wimbo wa 'Birthday'  yao, Mzee Mengi alizaliwa  Mei 29 na Abdiel alizaliwa Mei 28 na kuifanya siku hiyo muhimu kusherehekea pia siku yao ya kuzawaliwa.

Keki ikiandaliwa tayari kwa kukatwa.Nyuma kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Bi. Joyce Mhaville.

Dk. Mengi akikata keki. Kitendo pia kilifanywa na Mwanaye Abdiel.


Ze Comedy wa EATV waliweza kulimiki jukwaa kwa kuimba nyimbo mbalimbali na kuwapagawisha watu.

Haya sebene kwa kwenda mbele... Farouq Karim, Yvone Msemembo na Romana Mallya (kushoto) wakiserebuka.

Crew ya EATV wakiwa na Zahir Ally Zoro na Abdallah Bawazir (wa pili kushoto).

Kutoka Kushoto: Bawazir, Zahir Ally Zoro na John Badi


Mambo ya Mduara hayao...
Hellen Mwango naye aliamua kuonyesha mikiki yake.

Baada ya mambo kuchanganya wengine waliona viatu vizito wakaamua kuviweka kando ili wasebeneke vizuri.

No comments: