Tangazo

June 22, 2012

UKATILI:Mtoto Mchanga akutwa ametupwa akiwa amefariki jijini Mbeya - Kumradhi kwa picha hizi


 Maiti ya kichanga ambaye hayafahamika mama yake imekutwa imetupwa karibu na Msikiti wa Soweto Mbeya Asubuhi hii.


Picha ya juu na hii ya chini ni baada ya mtoto huyo kufumuliwa kutoka kwenye mfuko huo wa sulphate unao onekana akiwa amesha fariki, Hiyo nguo ni msamalia mwema ametoa.

Katika hali ya kutatanisha wananchi wa Soweto jijini Mbeya wamekutana na Kifurushi ambacho ndani yake kulikuwa na mtoto mchanga amewekwa na kutupwa akiwa amefariki, ikiwa ni tukio la pili kutokea eneo hilo baada ya tukio kama hilo kutokea wiki mbili zilizopita.

 Hata hivyo akiongea na baadhi ya wananchi ambao hawakupenda kutaja majina yao wamedai kwamba kuna dispensary jirani hapo ambayo hawakutaka sema ni hospital ipi ambapo wana wasi wasi kwamba hutoa Mimba mabinti na kuwatupa eneo hilo.

Mbeya yetu tunafanya uchunguzi wa kina kama ni kweli maelezo ya wadau na tunafuatilia kama kweli Dispensary hiyo ipo. Picha zote na Mbeya yetu Blog




No comments: