Tangazo

July 30, 2012

Airtel Tanzania yaendelea kusambaza Mawasiliano Kanda ya Ziwa-Mwanza

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh Charles Kitwanga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mawasiliano uliojengwa na Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, wakwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando. hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.

•  Mtandao huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke.

Airtel Tanzania imezindua mtambo kabambe wa mawasilano katika mkoa wa kanda ya Ziwa nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ikiwa ni mkakati wa Airtel uliojiwekea katika kuendelea kufikisha huduma zao bora  vijijini.

Akizindua mnara huo mpya Naibu mwishoni mwa wiki Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Raisi Mhe, Charles Kitwanga (mawe matatu) amesema Maendeleo vijijini yatakuwakwa kasi sana iwapo wananchi watatumia mawasiliano ya simu za mkononi kutafuta masoko ya madini, mifugo au vyakula wanavyozalisha  sehemu mbalimbali.

Waziri Kitwanga alibainisha hayo katika kijiji cha Nyamayinza kata ya Gulumungu wilaya ya Misugwi Mkoani Mwanza wakati akiongea na wananchi na kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya Airtel Tanzania.

Alisema “Mawasiliano yanafaida kubwa sana duniani na ndio hufanya maendeleo ya jamii kwenda kwa kasi, hivyo wananchi wa vijiji vyote vinavyoizunguka nyamayinza tumieni fulsa ya kupata mawasiliano haya ya Airtel kwa kuendesha au kuendeleza biashara zenu,pia anzisheni biashara za kutuma na kupokea pesa za Airtel Money  na mtumie mawasiliano haya haya pia kutafuta wateja wakutosha katika bidhaa za kilimo na mifugo mnazozalisha”

No comments: