Na Hirondelle, Arusha
Marekani imerudia msimamo wake wa kusaidia juhudi za kuwasaka watuhumiwa tisa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ambao bado hawajatiwa mbaroni na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).
Msimamo huo umerejewa na Balozi wa Marekani anayeshughulikia Uhalifu wa Kivita, Stephen Rapp katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu, makao makuu ya mahakama hiyo,mjini Arusha, Tanzania.
Rapp alisema Marekani itaendeleza mpango wake wa ‘’Zawadi kwa ajili ya Haki’’ ambao humpatia kiasi cha fedha hadi dola milioni tano za Marekani mtu yeyote anayetoa taarifa zinazosaidia kutiwa mbaroni mtuhumiwa ambaye bado anasakwa.Balozo huyo pia amedokeza kwamba mpango huo pia unaweza kutumika kwa watuhumiwa wanaotafutwa pia na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).
Watuhumiwa wakuu watatu wanaosakwa vikali na ICTR ni pamoja na Felicien Kabuga anayesadikiwa kuwa ndiyo mfadhili wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Rwanda,Augustin Bizimungu na aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Rais, Protais Mpiranya.
Iwapo watatiwa mbaroni watuhumiwa hao watatu kesi zao zitashughulikiwa na chombo maalum kilichoundwa kurithi kazi zitakazoachwa na ICTR kijulikanacho kwa jina International Residual Mechanism (IRM) tawi la Arusha na kilianza kazi rasmi Julai 1, 2012.
‘’Serikali ya Marekani bado inaendelea kujitoa kwa thati kuwafikisha watuhumiwa hawa mbele ya vyombo ya haki,’’ Rapp alisisitiza.
Kadiri ICTR inavyojitahidi kukamilisha majukumu yake,imeshaanza kuhamishia nchini Rwanda majalada ya watuhumiwa sita ambao bado wanasakwa ili kesi zake zikashughulikiwe nchini humo.Alisisitiza kwamba ni muhimu kwa watuhumiwa hao kukamatwa na kupelekwa Rwanda.
Akizungumzia hali tete ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rapp alitoa wito wa kukamatwa kwa viongozi wa waasi,Bosco Ntaganda na Sylvestre Mudacumura ambao wanatakiwa na ICC kwa uhalifu wa kivita. Alionya dhidi ya vitendo vya kuunga mkono kundi la waasi linaloongozwa na Ntaganda la M23 ambalo hivi sasa linapambana na majeshi ya serikali ya DRC.
‘’Marekani imekuwa ikiiambia mara nyingi serikali ya Rwanda,kusikitishwa kwake na vitendo vya Rwanda kuunga mkono kundi la waasi la M23 kama ilivyoaanishwa katika ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa,’’Rapp aliwaambia waandishi wa habari.
Alionya kwamba wafadhili wa mapigano hayo wanaweza kuwajibishwa kwa vitendo vyao.’’ Kama msaada unatolewa kwa vikundi vya wapiganaji na vikundi hivyo vikatenda uhalifu, kama wanashambulia miji na kusababisha watu kuuawa na kuleta vurugu na ubakaji, waliowapatia silaha na kuwaunga mkono wanaweza kuwajibishwa, na huu ni utaratibu muhimu,’’ alisema Rapp.

No comments:
Post a Comment