Tangazo

October 12, 2012

Deutsche Welle wamuaga Othman MirajiBaada ya miaka 35 ya utumishi wa uaminifu katika Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, Othmani Miraji  Ijumaa leo 12.10.2012, ilikuwa siku yake ya mwisho kazini kama Mhariri Mwandamizi.

Wafanyakazi wenzake, wakiongozwa na Mhariri Mkuu wa DW, Bibi Ute Shaeffer na Mkuu wa Matangazo ya Kiswahili, Bibi Andrea Schmidt, walimfanyia karamu murua ya kumuaga na kumtakia kila la heri na afya njema katika maisha yake ya baadae.

Pia walisifu mchango mkubwa alioutoa katika kuifanya DW iwe kuinganisho cha kupata habari za kuaminika na moto moto kutoka duniani kote na katika kuikuza lugha ya Kiswahili.

 Othman Miraji alijiunga na DW akitokea idara ya kunasa matangazo ya BBC Monitaring service, Nairobi, Kenya, mwaka 1977 ambako alitumika kwa miaka saba.

No comments: