Tangazo

October 29, 2012

USIKU WA MWANAMKE MJASIRIAMALI WAFANA


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete katika Hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali ya kuchangisha fedha kwa Wanawake Wajasiriamali ikiwa ni Kipindi cha Mwezi wa Wanawake Wajasiriamali nchini wenye Kauli mbiu "Msichana Amka Ujasiriamali ni Ajira" ambapo amewataka Wakinamama waliokwisha fanikiwa kuwaongoza Wasichana na wajasiriamali wanaochipukia njia sahihi za kibiashara zitakazowawezesha kufikia mafanikio katika biashara na kutumia ubunifu wao kama rasilimali.

Pia amewataka Wanawake kuonyesha Upendo na kushirikiana kwani Wanawake ndio chanzo cha Maendeleo katika Taifa lolote.

Mjasiriamali na Mkufunzi Bi.Namsifu Nyagabona akishirikishana uzoefu wa Biashara na wanawake wajasiriamali katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali iliyohudhuriwa na Wabunge Wanawake pamoja na Wake za Viongozi uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.

Mjasiriamali Rhoda Mwamunyange akitoa hamasa kwa wanawake katika Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali ulioandaliwa kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake Wajasiriamali ulioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) pamoja Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).
Mtaalam wa Saikolojia na Ushauri Aunty Sadaka Ghandi akizungumza katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali ambapo amewasisitiza Wanawake pamoja na Masuala yote ya Msingi pia waangalie uwiyano baina ya Familia na Biashara ambayo inaleta kipato katika Familia ili kuepukana na madhara ambayo yanaweza kuwapata wanafamilia kutokana na kujali sana kipato na kusahau Ulezi wa Familia.
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Marvelous Flotea Ltd. Bi. Flotea Massawe wa Kampuni inayojihusisha Handcraft Textile, Gift Accesories, Home Textlite na Food Processing akizungumzia jinsi alivyoanza kwa kufanya biashara ya kutandika Batiki chini maeneo ya Mnazi Mmoja na kuibuliwa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) kupitia kitengo cha kuwawezesha wajasiriamali ambapo mpaka sasa biashara zake ni nchini na nje ya nchi zilizomwezesha kupata tuzo mbalimbali za Kimataifa katika biashara.

Aidha amewataka Wanawake wanaochipukia katika ujasirimali kutokata tamaa na kuwa na ubunifu na uthubutu katika biashara kwa sababu usaidizi upo utakaowawezesha kutambulisha biashara zao ndani na nje ya nchi.

Meza kuu ikisikiliza Shuhuda za Kinamama waliofanikiwa katika Biashara za Ujasiriamali. Mgeni rasmi katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasirimali Mama Asha Bilal (wa tatu kulia), Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda( wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA Bi. Hulda Kibacha (kulia), Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Therezya Huvisa (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Taasisi ya MOWE Bi. Elihaika Mrema (wa tatu kushoto).

Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya Wake za Viongozi, Wabunge Wanawake na Wanawake Wajasiriamalia waliohudhuria hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali iliyofanyika jijini Dar es Salaam Serena Hotel.

Meza kuu ikipiga makofi kuwapongeza Wanawake wajasiriamali waliotoa mada na waliofanikiwa na kuwezesha kwa kufanyika hafla hiyo ambayo ni mfano wa kuigwa.

No comments: