Tangazo

November 9, 2012

KONYAGI YAKABIDHI MSAADA WA VYOMBO VYA MUZIKI KWA MSONDO NGOMA

Kiongozi wa Msondo Ngoma, Said Mabela akipokea sehemu ya vyombo vya muziki kutoka kwa Boss wa Konyagi, David Mgwasa (wa pili kulia).
Na Mwandishi Wetu

BENDI kongwe nchini ya Msondo Ngoma imekabidhiwa vifaa vya muziki na kampuni ya Konyagi Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi nchini, David Mgwasa alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania na kuifanya msondo kuwa imara katika kutoa burudani kwa watanzania.

"Msondo ni bendi kongwe tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 imesimama imara katika kutoa burudani ya uhakika kwa watanzania sanjari na kutumia nyimbo zake katika kuelimisha, kufunza jamii ya watanzania walio wengi," alisema Mgwasa.

Alisema watu wengi kwa kuwepo bedndi ya msondo wamewezakupata mafunzo mengio kupitia nyimbo zao ambazo nyingi zimekuwa zikitoa mafunzo kwa watanzania.

Hivyo alisema kuwa kwa kuwapatia vifaa hivyo, Msondo itakuwa moto wa kuotea mbali katika kutoa burudani ya uhakika hali itakayofanya bendi nyingine kwa wasindikizaji katika tasnia ya muziki wa dansi nc?hini.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Maalim Gurumo alisema kuwa kwa sasa wanadeni kwa Watanzania na kampuni ya Konyagi katika kutoa burudani ya uhakika baada ya kupatiwa vifaa hivyo.

"Tunaamini baada ya leo kupata vifaa hivyo tutatoa burudani ya uhakika sanjari na kukijenga vyema kikosi chetu kwa lengo la kukiimarisha," alisema Gurumo.

Kiongozi wa bendi hiyo Said Mabela alitoa shukrani wa kampuni ya konyagi kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kutoa burudani safi kwa Watanzania na Afrika kwa ujumla.

"Tunashukuru kampuni ya Konyagi kutupatia vifaa vya muziki ambavyo kwetu ilikuwa ni vigumu kwa kipindi hiki kuvipata, hivyo tunaamini tutafanya tutaendela kuwa vinara katika kutoa burudani nchini," alisema Mabela.

Ofisa Habari wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa amefurahishwa na kampuni hiyo kutoa vifaa hivyo akiamini kuwa vijana wake watafanya vizuri zaidi katika ushindanio wa muziki huo nchini.

Pia aliwaomba wadau wengine wa muziki nchini kujitokeza  kuisaidia Msondo ili kuijengea uimara katika ushindi wa muziki huo nchini ili kuendelea kuwa bendi bora na ya kuigwa nchini.

No comments: