Tangazo

April 17, 2013

Bondia 'King Class Mawe' ajifua kumkabili Bondia Amosi Mwamakula

Kocha wa Mchezo wa Masumbwi Nchini,  Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto), akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi ya kupiga masumbwi na kupangua ngumi za mpinzani wake.
########################

Bondia Ibrahim  Class 'King Class Mawe' amendelea kujifua na kujiandaa kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.

Pambano la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam siku ya Mei Mosi na linatarajiwa kuwa la vuta nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.

Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa bondia wake anajiandaa vema na matumaini yanaonekana baada ya kucheza Sparing na watu watano tofauti tofauto ambapo alianza kupambana na Abuu Mtambwe raundi 4, Kassimu Gamboo, nae vile vile na Ibrahimu Toll pamoja na Ally Masaga kitu ambacho kimenipa moli wa kumchakaza Mwamakula ili kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.

"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema Super D.

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali

No comments: