Tangazo

April 15, 2013

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA, MARGARETH THATCHER

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Melrose, wakati alipowasili kwenye Ofisi za Ubalozi huo, zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Waziri wa zamani wa Uingereza, Margareth Thatcher, aliyefariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa Kiharusi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Bi. Margareth Thatcher, aliyefariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa Kiharusi. Makamu amesaini kitabu hicho kwenye Ofisi za Ubalozi wa Uingereza nchini zilizopo jijini Dar es Salaam.Picha na OMR

No comments: