Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar
Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza
kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema
Zanzibar. (Picha zote na Martin Kabemba)
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi
Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya
Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi Kuu za Chadema kisiwani humo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar
Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza
kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyoJumamosiAgosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema
Zanzibar.
Mbunge wa CAHDEMA viti Maalum wa CHADEMA
Mwanamrisho Abama akimdhamini Mgombe Ujumbe wa Kamati Kuu wa Chama
hicho Salum Mwalim katika ofisi za chama Zanzaibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisiza Chadema
Zanzibar.
Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA
kundi la Zanzibar akitia saini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi Kuu za chama hicho Zanzibar kwa lengo la
kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Na Martin Kabemba, Zanzibar
Mmoja wa wanahabari na mtangazaji
mahiri wa wakati huu Salum Mwalim ameomba kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia nafasi za Zanzibar,
Uamuzi huo wa Mwalim ambae kwa sasa ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya
Vodacom tayari umeibua mjadala Zanzibar na kwamba unatarajiwa kubadili upepo wa
uchaguzi wa Chadema Visiwani humo kutokana na ushawishi na mvuto alionao
utakaomfanya kukubalika na kuaminika huku akifanya joto la uchaguzi kupanda.
Kwa sasa joto la uchaguzi ndani ya
Chadema linaonekana kuwa juu zaidi Tanzania Bara.
Akichukua fomu ya kuomba kugombea kuingia kwenye chombo hicho kikuu cha maamuzi
ndani ya Chadema, Mwalim amesema baada ya kushawishiwa na watu wa rika na wa
aina mbalimbali kushauriana na makundi mbalimbali amejipima na kuona kuwa
anatosha katika nafasi hiyo.
Mwalim amesema wakati wote wa maisha yake amekuwa akitembea na uzanzibari wake
na kwamba alitambua kuwa siku moja atakuja kuwatumikia wazanzibar na hivyo
kutoa mchango wake katika maendeleo ya visiwa hivyo ambako ndiko asili yake
ilipo.
Mwalim amechukulia fomu hiyo mapema leo (Jumamosi Agosti 30) katika ofisi kuu
za Chadema Zanzibar na kuirudisha majira ya mchana ikiwa leo ndio siku ya
mwisho ya uchukuaji wa fomu na urejeshaji kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
ndani ya chama hicho,
"Nimechukua fomu na sasa nairudisha, kwa kuwa wakati wa kampeni bado
sitoweza kuzungumza wala kujinadi naomba niheshimu taratibu na miongozo ya
uchaguzi ya chama lakini nataka kuwaambia kuwa Zanzibar na U-zanzibari wangu ni
jambo ninalojivunia kuliko kitu kingine chochote maishani mwangu."Alisema
Mwalim
"Ni uamuzi mgumu sana kuwahi
kufanya katika maisha yangu lakini nimeufanya kwa kuzingatia masilahi mapana ya
chama ninachokiamini na kwa nchi yangu ya Zanzibar na watanzania kwa
ujumla,ninamuomba Mwenyezi Mungu anisimamie anipe nguvu,afya,hekima,busara,
unyenyekevu na uadilifu katika safari hii ya siasa ninayoianza." Aliongeza
Mwalim
Akiongea kwa kujiamini na kwa umakini mkubwa, amesema ana imani kubwa kuwa
ataungwa mkono na kushinda nafasi hiyo kwa kuwa pande zote mbili za Visiwani na
Bara wanamfahamu vizuri sana na wanatambua mchango wake kwa Chadema na kwa nchi
kwa ujumla.
Mwalim ambae ni msomi wa masuala ya uandishi wa habari na
mwenye shahada ya uzamii katika usimamizi wa Biashara ni mmoja wa vijana
waliotokea kujizolea umashuhuri mkubwa nchini kutoka na uwezo wake na uchapaji
kazi wake akiwa mtu mwenye misimamo na kukubalika hasa na vijana nchini.
Kamati kuu ya Chadema ndicho chombo kikuu cha maamuzi ndani ya Chama hicho, na
iwapo Mwalim atafanikiwa kushinda na kuingia kwenye chombo hicho anatabiriwa
kuwa atabadili upepo wa Chadema katika siasa za Zanzibar kutokana na
Mwanahabari huyo kukubalika katika jamii na upya wake katika siasa unamfanya
kuingia katika siasa pasi na kuwa na makundi hali itakayomwezesha kupewa ushirikiano
na kila mtu ndani na nje ya Zanzibar.
Akimkabidhi fomu hiyo Makamu
Mwenyekiti wa Zanzibar wa Baraza la Wazee La Chadema Bi Maryam Ahmed Omar
amempongeza Mwalim kwa uamuzi wake huo na kumtakia kila la kheri katika
uchaguzi huo.
Bi Omar amesema Chadema ya sasa
imeimarika kwa kiwango cha juu na kwamba uamuzi wa Mwalim ambae ni kijana
mzaliwa wa visiwani humo wa kuamua kugombea nafasi hiyo utasaidia kuongeza
nguvu ya kukiimarisha chama.
Tukio la uchukuaji wa Fomu wa Mwalim
limehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa
Jumbe, mbunge wa wa viti maalum wa chama hicho Mwanamrisho Abama miongoni mwa
viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho
No comments:
Post a Comment