Tangazo

October 16, 2014

Airtel yakarabati duka jingine kisiwani Zanzibar

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi akijiandaa kukata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la huduma kwa Wateja la Airtel kisiwani Zanzibar(Kushoto) Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kulia) Maneja wa Kanda ya Zanzibar Mariam Yussuf.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

•Wateja kufurahia ubora wa juu wa huduma kutoka Airtel kisiwani Zanzibar.


Airtel Tanzania  imefungua duka lake la kisasa  kisiwani Zanzibar lililopo mtaa wa Mlandege lenye uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku.

Ni duka la kisasa ambalo lipo karibu na  wateja lenye kurahisisha maisha ya wateja wote wa Airtel kisiwani Zanzibar.

Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo Mkurugenzi kwa huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba alisema, "kwamba kupanua  kwetu kwa huduma za mtandao kwa wateja wetu ni ishara  tosha ya kuonyesha ni jinsi gani Airtel inajali wateja wake na kuwapatia wateja wetu huduma bora na za
kibunifu.

"Ni juhudi zetu  na  mafanikio yetu ya kuwa na wateja zaidi ya milioni 9 tulionao ndio yanayotufanya tuweze kuwashukuru wateja wetu kwa kuwapatia huduma nzuri zenye Kiwango cha juu. Kwa huduma unazozitoa kupitia maduka yetu yaliyoenea hapa nchini maduka haya yanauwezo wa kutoa huduma zenye kiwango cha juu  yanayotoa huduma kwa masaa mengi na kutoa huduma nzuri kwa wateja. Uzinduzi wa maduka yetu ni mafanikio makubwa kwetu na hii ni shukurani yetu kwao kwa kuwaonyesha ni jinsi gani tunawajali wateja wetu.

Hafla hiyo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa  Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi, ambaye aliipongeza Airtel kwa ajili ya kuleta huduma zake karibu na watu wa Zanzibar.


"Mbali na kutatua matatizo ya wateja, mtazamo huu mpya wa duka hili ni maendeleo tosha kwa wakazi wa Zanzibar kwani huduma zinazotolewa hapa ni za kiwango kizuri na uwezo mkubwa ambapo wateja wa Airtel wamekuwa wakihitaji hapa kisiwani Zanzibar. alisema.

Mwinyi alisema kuwa, huduma mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na Airtel kuanzia , ujumbe, Inteneti , usajili, huduma za Airtel Money ambazo zinarahisisha maisha ya wananchi katika jamii.



"Huduma hizi zinaleta matokeo mazuri katika namna ya kufanya biashara na kuboresha maisha ya maelfu ya wakazi wa Zanzibar na mamilioni ya Watanzania kwa ujumla," aliongeza Mwinyi.

Kama sehemu ya huduma nzuri , Airtel tayari imekarabati maduka mengine katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Bukoba, Mbeya, Mtwara, Dodoma, Mwanza, Tabora na leo hapa Zanzibar.

Maduka ya Airtel  yataendelea kutoa huduma mbali mbali zenye kiwango cha juu na upatikanaji wa bidhaa zake kama vile modems, simu, malipo ya bili,huduma za Airtel money na huduma nyingine nyingi .

Tumewekeza kwa kiwango kikubwa  katika mtandao wetu ili kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma sahihi na ya kiwango cha juu.

No comments: