Tangazo

October 16, 2014

KATIBU MKUU HAZINA NA UJUMBE WAKE NCHINI MAREKANI

KatibuMkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali, Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazo pendekezwa na Benki ya Dunia kwa mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier.
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu na kutoka kushoto ni  Bi. Natu Mwamba Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania wakimsikiliza kwa makini Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi hayupo kwenye picha, alipokuwa akijibu hoja zilizowekwa mezani.
Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali na kuahidi kuzifanyia kazi. Picha zote na Ingiahedi Mduma – Washington DC.

No comments: