Bendi Kongwe ya Muziki wa Dansi hapa nchini iliyodumu kwa miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1964,Msondo Ngoma Music Band imesherehekea jubilei yake hiyo iliyofanyika Novemba 1,2014 katika viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha mashabiki wake lukuki kutoka sehemu mbali mbali.
Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo ya kusherehekea Jubilei ya miaka 50 ya Bendi ya Msondo Ngoma,alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye aliweza kuwatunuku vyeti vya heshima wanamuziki mbali mbali walioitumia Bendi hiyo toka ilipoanzishwa mpaka sasa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.Picha Zote na Othman Michuzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima mpiga solo hodari wa Bendi ya Msondo Ngoma,Abdul Ridhwan "Panga mawe"
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akimkabidhi Cheti pamoja na fedha taslim sh. Laki 5,Mke wa Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo katika hafla hiyo ya kutimiza miaka 50 ya kuanziswa kwa Bendi hiyo.
Mmoja wa Waanzilishi wa Bendi hiyo,John Simon (Kapten Mstaafu) akizungumza machache pamoja na kutoa historia fupi ya kuanza kwa bendi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti pamoja fedha taslim sh. Mil. 5,Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) kwa niaba ya baba yake.
Mtangazaji Mkongwe hapa nchini na mwenye historia na Muziki wa Tanzania,Masoud Masoud (kulia) akionyesha moja ya CD za bendi ya Msondo Ngoma zilizokuwa zikinadiwa kwenye sherehe hizo mbele ya Wadhamini.
Safu ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede (katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
Mpiga Tumba wa Msondo Ngoma akifanya yake.
Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) akionyesha uhodari wake kiasi kwamba hata pengo la mzee wake kuhisi limezibwa.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.
Baba la Mababa,Mzee Said Mabela akiendeendelea kuzikonga nyoyo za Mashabiki wa Msondo.
Abdul Ridhwan "Panga mawe"
Shaaban Dede akiimba kwa hisia.
Juma Katundu.
Mkaanga chipsi wa Msondo akizicharaza kweli kweli.
Wakongwe wengine hawa wakiimba wimbo wao wa Tanzania.
Ilifika zamu ya Twanga Pepeta na huyu si mwingine bali ni Saleh Kupaza.
Kalala Junior.
Kalala na Msafiri Diof wakienda sawa na Mashabiki wao.
Msafiri Diof.........
Taswira juu ya Taswira katika Sherehe za Miaka 50 ya Msondo Ngoma.
Kalala Junior na Saleh Kupaza wakifanya yao ikiwa ni sehemu ya Usindikizaji wa Sherehe za Miaka 50 ya Msondo Ngoma.
Madansa wa Twanga Pepeta Juu kwa Juu
Mandela wa Twanga Pepeta
Wacheza Shoo wa Twanga Pepeta ni Hatariiiiiiiii...
Wadau wakijipatia taswira muhimu.
Msondo Umekolea kwa Mdau huyu.
Wadau.
Romariiiiiiiiiii Romariooooooo na Trampet yake.
Mdau akichukua taswira muhimu.
Dar Modern Taarab "watoto wa mjini" wakisindikiza sherehe hizo.
Msondo Ngoma iliyozikonga nyoyo za Mashabiki wao hakuna mtu kukaa chini.
Msongo Ngoma staili.
Bendi ya Vijana Jazz ilikuwepo kuwasindikiza kwakongwe wenzao.
Bint wa Kiongozi wa Bendi ya Vijana Jazz Marehemu Hemed Maneti akitoa burudani safii.
Hakuna kazi ngumu kama ya kupuliza hii kitu,inahitaji pumzi kubwa sana kama wanavyoonekana wanamuziki hawa wa Vijana Jazz.
Nyomiiii.
MC Zomboko.
No comments:
Post a Comment