Tangazo

February 25, 2015

WARSHA KUHUSU NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WATOTO NCHINI TANZANIA YAFUNGULIWA KILIMANJARO

 
 Julieth Swai Mwakilishi kutoka UNICEF akizungumza jambo
 Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia kwa makini
 Mmoja wa  washiriki wakiuliza maswali katika warsha hiyo
 Kimela Bila Mwandaaji wa Kipindi cha Walinde Watoto akizungumza katika Warsha hiyo
 Mathias Haule, Afisa Maendeleo ya Jamii maswala ya Ukatili dhidi ya Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akielezea Sheria ya Mtoto
 Neema Kimaro, Mratibu wa kipindi cha Walinde Watoto kutoka True Vision Production akiendelea na maandalizi ya warsha
Rose Minja, Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya familia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
akijibu maswali ya washiriki wa Warsha inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili
dhidi ya Watoto nchini Tanzania
 Wawakilishi kutoka redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde watoto

 Washiriki wa Warsha inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania
***
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF wameandaa warsha ya siku tatu inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.

Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, wawakilishi kutoka UNICEF pamoja na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

Wengine ni wawakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania, mwakilishi kutoka Csema pamoja na waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kampuni ya True Vision Production.

Akifungua warsha hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Shayo alilishukuru shirika la Watoto Duniani (UNICEF) kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakizifanya kwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa Haki za Watoto zinatekelezwa hapa nchini. 

Paul alitaja aina za ukiukwaji wa haki za mtoto hapa nchini kuwa ni pamoja na kuolewa katika umri mdogo, kutumikishwa katika mashamba na ukatili dhidi ya watoto. Hata hivyo aliendelea kuzitaja athari mbalimbali zinazotokana na ukiukwaji wa haki hizo kuwa ni pamoja na watoto kukatishwa masomo na kukosa haki ya kuendelezwa na kwamba ndoa za utotoni zina madhara kiafya hasa wanapopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo. 

Paul alimalizia kwa kutoa rai kwa washiriki wa warsha hiyo na kuwataka wakawe chachu ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto katika maeneo waliyotoka na kushirikiana na wadau waliopo katika ngazi za vijijini, mikoani na mijini kadri inavyowezekana ili kuwalinda watoto na kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.

Vipindi vya Walinde Watoto vinarushwa na redio 14 ambazo ni Radio Jamii Kilosa, Country FM, Boma Hai FM, Radio Quran, ZBC pamoja na Redio Kitulo.

Nyingine ni TBC Taifa, Bomba FM, Faraja FM, Uplands FM, Ice Fm, Radio Maria, Radio Kwizera na Zenj FM. Vipindi hivi vinapatikana pia katika tovuti ya www.walindewatoto.org na kupitia www.facebook.com/WalindeWatoto

No comments: