Tangazo

March 9, 2015

Airtel yaipiga 'Jeki' Bendi ya walemavu ya Tunaweza


Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akimkabithi Meneja wa Bendi ya walemavu ya Tunaweza Bwana Sixmond Mdeka mkataba wa udhamini wa kuredodi alibum yao ya muziki katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed (kulia) na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi mkataba wa udhamini kwa Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka, katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’ jijini Dar es Salaam, ambapo Airtel itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. Wanaoshuhudia ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed (wa pili kulia) na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

• Wawezeshwa kurekodi nyimbo zao mpya.

Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kwa watu wenye ulemavu,  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa udhamini kwa kikkundi cha muziki cha walemavu kijulikanacho kwa jina la “Tunaweza Band”, na kuwawezesha kurekodi nyimbo zao mpya.

Makabidhiano ya mkataba huo wa udhamini kati ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na Ontime Production yalifanyika katika ofisi za Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’ jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Meneja wa Kitengo chaHuduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi, alisema” msaada huo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya kijamii ambayo kampuni imeazimia kuifanya ikiwa na lengo la kuigusa jamii hususani ndugu zetu wenye ulemavu. Watu wanaoishi na ulemavu husahaulika katika jamii na hivyo tumeona ni vyema basi tuwawezeshe wanamuziki hawa wenye vipaji kuweza kufikia malengo yao na kuwapatia  uwezo wa kujiongezea kujiongezea kipato kutokana na vipaji walivyonavyo.

Ni matumaini yetu msaada huu utawewezesha kutoa album yao ambayo itawasaidia kujulikana katika anga za muziki wa bendi ndani na nje ya nchi na pia kupata kipato kupitia album hii itakayouzwa katika maeneo mbali mbali nchini. 

 Natoa wito kwa wananchi kuwaunga mkono kwa kununua album hii pindi itakapo kuwa tayari “Tunaendele kuona ni jinsi gani tutaendelea kuzigusa jamii mbalimbali kupitia shughuli zetu za huduma kwa jamii huku lengo likiwa ni kujikita zaidi katika kuchangia sekta ya elimu kupitia mradi wetu wa shule yetu. Tunaahii kuendelea kuzifikia shule nyingi zaidi nchini kwa mwaka huu wa 2015 huku tukiendelea kujikita katika kutoa vitabu na vifaa vya sayansi kwa shule zetu za sekondari,” aliongeza Hawa.

Naye  Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka alisema kuwa amefurahishwa na moyo wa kampuni ya Airtel  kwa kujali walemavu hapa nchini kwani wao si wa kwanza kupata msaada huu kutoka Airtel.

“Nimefurahishwa sana na kitendo cha Airtel kujali walemavu hapa nchini na kwa kutusiadia kuongeza vipaji vyetu na vile vile kutuwezesha kuongeza kipato chetu kwani baada ya hapa tunauhakika wa kupata mikataba ya kurekodi nyimbo zetu nyingine nyingi tu ambazo tunazo.

Kwa niaba ya  wenzangu wa kikundi cha Tunaweza, napenda kuwashukuru Airtel kwa moyo wao wa kujali watu walio katika mazingira magumu, hasa sisi walemavu. Msaada huu utatuwezesha kuendeleza bendi yetu na kutoa burdani kwa jamii katika maeneo mbalimbali na kutuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekea.

Mwishoni mwa mwezi wa Februari Airtel imewawezesha walemavu wengine kumi na tano kuweza kupata mafunzo ya biashara, mtaji na  vibanda vya kisasa vya Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel Money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

No comments: