Katibu Mkuu wa Mashindano ya Vyuo vilivyosajiliwa na NACTE
TANZANIA, Waziri wa Michezo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),
Ladslaus Tumbu (kulia) na Katibu Msaidizi wa Michuano hiyo, Waziri wa Michezo
kwenye Chuo cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Samweli Samweli (wa pili
kulia), wakikabidhi Kombe linaloshindaniwa na Vyuo mbali mbali Kanda ya Dar es
Salaam(Mashariki) kwa Viongozi wa NACTE, Msaidizi wa Mkurugezi, Alex Mkondola (wa
kwanza kushoto) na Mwanasheria Mkuu NACTE Cexemary Mize (wa Pili kushoto),
wakati wa hafla ya kukabidhi Kombe hilo la Michuano ya NACTE TANZANIA,
lililotolewa na Kampuni ya Simu za Mkononi VODACOM Tanzania, Michuano hiyo
inafunguliwa April 18 kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
XXXXXXXXXX
Kamati
ya Mashindano ya Michezo ya Vyuo Tanzania( NACTE INTER COLLEGE CHAMPIONSHIP
TANZANIA 2015), imekabidhi kombe la Michezo hiyo kwa Taasisi ya Elimu ya Vyuo
nchini Tanzania, NACTE baada ya kamati hiyo kupokea kombe hilo kutoka kampu ni
ya Simu ya VODACOM TANZANIA, lililotplewa kwa ajili ya michuano hiyo ya vyuo
vya Tanzania iliyoanza November Mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
makao makuu ya Wizara(NACTE) Msaidizi wa Mkurugezi, Alex Mkondola alisema kuwa ni
heshima ya pekee kwa NACTE kutokana na Uwepo wa michezo hiyo inayoshirikisha
vyuo mbali mbali vilivyosajiliwa na NACTE nchini Tanzania.
"Wanafunzi wengi vyuoni wamekuwa wakizungumzia hitaji lao
la kutaka michezo ya pamoja kwa vyuo vya elimu ya kati na vyuo vya elimu ya juu
kushindana katika kutafuta bingwa wa kila mchezo, hivyo fulsa hii ni yao na
sisi jukumu letu ni kuhakikisha kwamba michezo hii inafanyika kupitia
wasimamizi mwakuu tuliowapa ridhaa ya kuwa waandaaji kampuni ya Miss Demokrasia
Tanzania.
Ni matumaini yetu kwamba sasa vijana mbali mbali watashiriki
kujiandikisha kwa ajili ya kuonyesha Vioaji vyao bila kubagua aina ya mchezo,
tunashukuru wenzetu wa VODACOM wao kuwezesha Kombe hili kubwa kwa ajili ya
mchezo wa mpira wa Miguu, lakini hata hivyo michezo yote itashiriki isipokuwa
tunapenda kuwasisitiza wakuu wa vyuo kuwapa mwanya huo vijana wao waweze
kuwakilisha taasisi zao katika kuwania tuzo hizi ambazo zinatofautiana kutokana
na ubora wake, sisi kama NACTE tumeona ni jambo la kupendeza kuwapo kwa michezo
hii kwenye vyuo vya elimu ya kati na hata elimu ya juu ili mradi wawe wanachama
wetu, tunapenda tu kutoa angalizi kwa wakuu wa vyuo, kwamba tusingependa
wanamichezo wao kuonyesha nidhamu mbaya michezoni, maana lengo kubwa la michezo
hii ni kujenga mahusiano mema na siyo kuleta mgongano, na pia ni kwa ajili ya
kujenga afya zao wenyewe maana michezo inawajenga katika mambo mengi hivyo waitumie
fulsa hii kujenga mahusiano mazuri miongoni mwao, tuwashukuru wadhamini wote.
Waliojitokeza kusaidia baadhi ya mahitaji kwa ajili ha
kufanikisha michezo hii ya vijana wetu, na pia tuwatake wawezeshaji wengine
kujitokeza katika kusaidia wakati wote wa mashindano, kwa sasa NACTE imepanua
wigo maana tunayo matawi 6, Kanda ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Zanzibar na
Dar es Salaam, tunahitaji kupata bingwa wa Tanzania kwa College zilizo
mwanachama wetu, Siku ya ufunguzi tunaomba wakuu wa vyuo vyote vya Dar es
Salaam na maeneo ya jirani, kuruhusu wanafunzi kuhudhulia kwenye Kongamano
kubwa la Ufunguzi ambapo wanafunzi wote watapata fulsa ya kujiandikisha kwa
ajili ya kushiriki kwenye fani mbali mbali za vipaji vyao ikiwa ni pamoja na
Dibate" alisema Alex Mkondola
Michezo hiyo inazinduliwa April 18 kwenye viwanja vya Chuo kikuu
cha Dar es Salaam, ambapo jumla ya timu 18 zitashiriki kwenye ligi hiyo ambayo
imeingia hatua ya pili baada ya hatua ya kwanza ya makundi ya mtoano kumalizika
ambapo jumla ya vyuo 115 vilishiriki kabla ya hatua hii ya 18 bora.
Wadhamini waliokotpokeza mpaka sasa ni Vodacom Tanzania, Coca
Cola, EQUITY Bank, P.S.I, TBL, TTB, White Dent, Fastjet, , MSD,
N.H.I.F, CLOUDS MEDIA GROUP, FREE MEDIA, Tanzania Daima, MLIMAN TV & Radio,
Viasat 1 Tanzania( TV-1), Global Publishers, Michuzi Media Group, MpaluleBlog,
Event World, DACICO, Mliman Professional, Njuweni Institute of Hotel, Catering
& Tourism Management, Zinduka Development Initiatives Forum,Dkt Mwaka, BIG
BON, No-saspect Berbershop,CXC Tours, Omari Mawamba na Mlonge By Makai.
No comments:
Post a Comment