Tangazo

March 17, 2015

NHIF LINDI WATOA ELIMU KWA WANACHAMA WAKE KATA KWA KATA, SANJARI NA UPIMAJI WA AFYA BURE KWA WANANCHI WILAYANI RUANGWA


Meneja wa Ofisi ya mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akitoa mada ya maboresho yanayotekelezwa na mfuko hususani kitita cha mafao kwa wanachama katika kata namichiga  wilayani ruangwa ambapo pia aliwataka kutumia mkutano huo kubainisha changamoto hasi na chanya zitakazowezesha maboresho ya huduma za matibabu sambamba na sekta ya afya kwa ujumla. Kushoto katikati ni Mtendaji Kata ya Namichiga, Richard Nnonjela na (kushoto kabisa) ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Namkonjera iliyopo kata ya Namichiga.

Watumishi wa kada mbalimbali ambao ni wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya waliopo wilayani ruangwa katika kata ya namichiga wakimsikiliza meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya hayupo pichani wakati wa utekelezaji wa mpango wa elimu ya kata kwa kata sambamba na upimaji wa afya kwenye magonjwa yasiyoambukiza ambapo alisema yamekuwa ni ya gharama kubwa kwa kuwa wengi hawafahamu dalili zake hivyo uyafahamu wakati tayari yameshafikia hatua kubwa ya madhara na wakati mwingie kuchangia vifo,hivyo ofisi ya mkoa wa lindi umekuwa  ukitekeleza kwa nia ya kuongeza uelewa na wanaobainika kuwa na viashiria kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari wanaotoa huduma.

Bi. Aisha Manjurungu akipata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa Dk. Joyce Mmuni baada ya kupata vipimo ambapo  zoezi la upimaji afya bure kwa wanachama wa mfuko na wananchi umetekelezwa kwa kutoa huduma ya upimaji kwenye magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari,presha na uwiano wa uzito wa mwili na urefu,u katika viwanja vya gulioni kata ya namichiga.

Wananchi wakipata huduma ya upimaji kwenye banda la mfuko pichani dkt.grolia kiria akimpima bp mmoja kati ya mwananchi aliyefika kupata huduma zilizokuwa zikitolewa mbali na upimaji wananchi walihamasishwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF).

No comments: