Tangazo

September 6, 2015

MGODI WA DHAHABU, BULYANHULU WATUMIA NUSU BILIONI KWA MWAKA KUFADHILI VIJANA MAFUNZO YA IMTT

 Meneja Ufanisi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Elias Kasikila, (kushoto), akiagana na baadhi ya vijana wanaokwenda kuhudhuria mafunzo ya ufundi chini ya mpango wa IMTT unafadhiliwa na mgodi huo, wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye eneo la mgodi, huko Msalala mmoani Shinyanga. Mgodi huo umetuamia kiasi cha zaidi ya  nusu bilioni kila mwaka kufadhili mpango huo

Na K-VIS MEDIA

MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini ya Acacia, umetumia kiasi cha zaidi ya shilingi nusu bilioni kila mwaka, kufadhili mafunzo ya ufundi kwa vijana, chini ya mpango wa IMTT.

Mpango wa kufadhili mafunzo ya IMTT, (Integrated Mining Technical Training), ulianzishwa mnamo mwaka 2009, ambapo mgodi huo hutoa fedha kufadhili elimu hiyo kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne ambao walisoma kwenye shule zilizoko vijiji 14 vinavyozunguka mgodi huo na kushindwa kuendelea na kidato cha sita kwa sababu mbalimbali lakini wawe na umri usioozidi miaka 25.

Akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga vijana 20 kutoka vijiji hivyo kwenye mgodi huo, mwishoni mwa wiki ambao wameenda kuanza mafunzo hayo yanayochukua muda wa miaka kati ya mitatu na miwili kwenye chuo cha VETA-Moshi, Menenja Ufanisi (OE),wa BGML, Elias Kasikila, alisema, ufadhili huo ni utekelezaji wa sera ya mgodi kushirikiana na wenyeji wao, (wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mgodi), katika kujenga mahusiano mema.

Akielezea utaratibu wa kuwapata vijana hao, Kasikila alisema, waombaji hupeleka maombi yao kwenye ofisi za serikali za vijijina kisha maombi hayo kukabidhiwa kwa uongozi wa mgodi ambao huyaachuja kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

“Sharti muombaji awe amefaulu masomo ya Kiingereza na Hisabati, lakini kupitia kitengo chetu cha usalama, vijana hao huchunguzwa tabia zao huko walikotoka, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya kiafya na wanaokidhi vigezo hivyo huchaguliwa.” Alifafanua

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na ufundi umeme kwa miaka mitatu, fitting na uchomeleaji vyuma, kwa miaka miwili, Diesel mechanic and Instrument, kwa miaka mitatu. Alifafanua Kasikila.
“Kila kijana tunamlipia shilingi milioni 7 kwa mwaka ambazo hutumika kama ada, malazi, ununuzi wa vitabu na vifaa, lakini pia tunawapatia shilingi 100,000 kwa kila kijana kila mwezi ikiwa ni kitunza mfuko kwa matumizi madogomadogo bila kusahau usafiri wa kwenda na kurudi kutoka chuoni.” Alisema Meneja huyo.

Kasikila alisema, vijana 64 waliotokana na mafunzo hayo wamepata ajira ya kudumu, 59 kwenye migodi inayomilikiwa na kampuni ya Acacia, na watano (5), wameajiriwa na mgodi wa Geita Gold Mine, GGM), huku wengine 89 wanafanya kazi mafunzoni, (trainees).
“Lengo kuu la mafunzo haya sio kutoa ajira kwa vijana hawa, bali ni kuwajengea uwezo wa kujiajiri  wengine na wachache huwa tunawachukua lakini pia huwa tunawaunganisha na taasisi nyingine zinazohitajio utaalamu wao.” Alifafanua Kasikila.

Akitoa shukrani kwa niaba ya vijana wenzake, Baraka Nasoro, aliushukuru mgodi huo kwa kuwawezesha kupata fursa ya kielimu na kuwaasa wenzake kujituma ili hatimaye kumaliza masomo kwa mafanikio.

Naye mwakilishi wa wazazi wa vijana hao, Rhoda Aaron, amewataka vijana hao kujiepusha na vitendo vya anasa na uasherati ili waweze kushiriki vema mafunzo na kuzingatia kilichowapeleka
 Maafisa wa BGML, wanaosimamia mpango wa IMTT
 Kasikila akitoa nasaha zake
 Baadhi ya vijana waliofaidika na IMTT mwaka huu wakisiliza kwa makini nasaha zilizokuwa zikitolewa na uongozi wa BGML, na wazazi wao
 Wazazi wa vijana waliofaidika wakisikiliza


 Mmoja wa wazazi wa vijana hao, Rhoda Aaron, akitoa shukrani zake na nasaha kwa vijana
 Kasikila, (kulia), akipongezwa na Rhoda
  Maafisa wa BGML, wanaosimamia mpango wa IMTT
Mwakilishi wa vijana hao, Baraka Nasoro, akitoa shukrani zake kwa niaba ya wenzake.

No comments: