Dar es Salaam,
Siku chache baada ya
kuachia video ya wimbo wake - ‘NINGEFANYAJE’, muimbaji wa R&B
kutoka Tanzania, Bernard Paul maarufu kama Ben Pol ameeleza
sababu zilizopelekea muimbaji Avril kutoka Kenya
aliyeshirikishwa kwenye wimbo huo, kutoonekana kwenye video hiyo
anayoitaja kuwa kubwa kuliko video zote alizowahi kufanya.
Katika video hiyo
iliyoongozwa na Justin Campos wa Afrika Kusini, Ben Pol anaonekana
akiimba na Rossie M ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo huo huku
mashabiki wakiisikia sauti ya Avril bila kumuona mwimbaji huyo
mrembo.
Ben Pol amewaomba
radhi mashabiki wake kwa kuwapa video ambayo haijakamilisha wahusika wote
hususan kutokuonekana kwa Avril, na kwamba sababu
zilizopelekea hivyo zilikuwa nje ya uwezo wa pande zote katika utayarishaji wa
video hiyo.
Ben amesema kuwa baada ya yeye na Rossie M kuwasili Afrika Kusini
ilikoshutiwa video hiyo, zilijitokeza changamoto muda mfupi kabla ya kuanza
zoezi hilo. Ben Pol ameeleza kuwa pamoja na kuwa na maandalizi makubwa,
video ya‘Ningefanyaje’ ilikumbwa
na changamoto nyingi tangu awali zilizopelekea kuahirishwa mara tatu.
“Kwa kweli hii video tokea mwanzo
ilikuwa na changamoto, kwanza tuliisogeza mbele karibu mara tatu tena tukiwa
tayari tumeshafika Afrika Kusini mimi na Rossie,” alisema Ben Pol.
“Mara ya kwanza ni kutokana na ‘delay’ ya viza upande waAvril. Si unajua
Wakenya wao wanaenda South kwa viza tofauti na sisi Tanzania hatuendi kwa viza
so kwetu ni rahisi zaidi muda wowote tu ukiamua fasta unaenda,” aliongeza.
Mkali huyo alieleza kuwa baada ya
terehe mpya kupangwa na muongozaji aliyeshuti video hiyo, Justin Campos, siku
moja kabla ya kushuti, AVRIL alipata tatizo lingine ambalo lilimzuia kusafiri
kwa siku iliyofata kwenda Afrika Kusini.
Wakati huo huo, Campos naye
alimueleza Ben Pol kuwa kwa jinsi ratiba yake ilivyo
endapo ataahirisha tena kushuti video hiyo, ratiba yake isingemruhusu kushuti
video hiyo hadi Januari au Februari 2016, kitu ambacho Ben Pol amesema
kisingewezekana kwasababu ingeendelea kumgharimu zaidi kifedha na kuvuruga
‘timing’ yake.
“Kutokana na hali hiyo, sikuwa na
jinsi nyingine zaidi ya kukubali matokeo kwasababu mwisho wa siku si mimi
wala Avrilwala director aliyekwamisha bali ni ‘situation’ ambayo
ilikuwa nje ya uwezo wa kibinadamu.” Ben Pol anaeleza.
Ameongezea kuwa pamoja na
kwamba angeweza kuamua kushuti video kwa kutumia version nyingine ya wimbo huo
isiyokuwa na sauti ya Avril ili video isionekane na upungufu
wake, lakini hakupenda kufanya hivyo kwa kuwa lengo kuu la wimbo lilikuwa
kumshirikisha mwimbaji huyo. Pia, mashabiki wangekosa ladha nzuri na kazi nzuri
aliyoifanya Avril. Hivyo, aliamua kufanya video hiyo
bila Avril na kukusudia kuwaeleza mashabiki wake
kilichosababisha hali hiyo kwa kuwa aliamini mashabiki wataelewa magumu
aliyopitia katika kuwapa video hiyo waliyokuwa wakiisubiri.
“Namshukuru sana Avril kwa
kukubali kufanya kazi na mimi kwasababu imetimiza moja kati ya malengo yangu ya
2015, ambayo ilikuwa kuanza kufanya kazi na wasanii wa nje ya Tanzania na yeye
ndiye alikuwa chaguo langu la kwanza. Ni imani yangu tutafanya tena project
nyingine ya pamoja na kuikamilisha kama tulivyoikusudia,” alimaliza Ben
Pol na kuwashukuru mashabiki wake kwa kuupokea kwa mtazamo
chanya wimbo na video yake.
Tazama ‘NINGEFANYAJE’ YouTube: https://youtu.be/iuUdNwR06BE
No comments:
Post a Comment