Mmoja wa watangaziji mahiri wa kituo cha EFM redio Gadner G Habash
akitumia kadi ya kwanza kutolewa mara baada ya Airtel na Total kuingia ubia na
kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo
ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. Anaemuhudumia ni mtoa huduma wa
Total, Bi Saumu Othmani (kati) na Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar
es Salaam
Kampuni ya
simu za mkononi ya imeingia ubia wa kibiashara na kampuni ya kimataifa nchini
ya TOTAL inayojihusisha na kuuza mafuta ya magari pamoja na bidhaa za
vilainisha ingini na mitambo, Ushirika huo wa Airtel wa Total ni kupitia huduma
ya kifedha ya Airtel Money wenye lengo la kuwawezesha wateja wao kutumia kadi
ya kugusisha ijulikanayo kama ‘AIRTEL MONEY TAP TAP’ kufanyia malipo yabidhaa
katika vituo vyote vya Total .
Kadi ya
Airtel Money ya Tap tap imeunganishwa moja kwa moja na akaunti ya Airtel money ya mteja ili mteja aweze kuitumia
mahali popote anaponunua bidhaa yoyote katika vituo vya Total nchini. Kutokana
na ushirika huo wateja wote wa Airtel na Total watafurahia kupata huduma zote kwa
usalama zaidi bila kulazimika kubeba pesa taslimu.
Huduma hii
ya kadi ya malipo kwa kugusisha ya Airtel
Money Tap tap imetokana
na ugunduzi wa utafiti wenye dhamira ya kuendelea kutumia teknolojia za kisasa
ili kuwezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi na usalama zaidi. Mteja
atagusisha kadi tu kwenye kifaa maalumu cha kufanyia malipo na kulipa papo hapo
baada tu ya kuingiza namba yake ya siri ya Airtel Money, teknolojia hiyo
inajulikana kwa lugha ya kiingereza kama (Near Field Communication)
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja wa Huduma ya Airtel Money Tap tap hiyo
Bw, Stephen Kimea alisema “tunajisikia fahari sana leo kuingia ubia na Total
ili kuwaweze wateja wetu kufaidi kutumia huduma ya Airtel Money Tap tap. Hii ni huduma yakwanza kutolewa nchini Tanzania na
Airtel ili kuboresha usalama zaidi kwa wateja pale wanapofanya malipo ya huduma
na bidhaa mbalimbali. Kila kwenye kituo cha Total wateja wetu wataweza kutumia
kadi hii, lengo letu ni kufanya wateja wetu wafurahie huduma zetu zaidi”
Kimea
aliendelea kueleza “Airtel tutahakikisha kuwa huduma hii ya kufanya malipo kwa
kutumia kadi yaAirtel Tap tap inapatikana
kwa wafanyabiashara na watoa huduma wakubwa na wakati zaidi ya elfu 25 nchini,
hii nikutaka kutoa suluhisho la usalama wa raia kwa kuondokana na tatizo la
kubeba pesa nyingi wanapokwenda kufanya manunuzi na badala yake sasa watatumia
kadi hii”
“sasa kadi
hizi zitapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya Total na katika baadhi
maduka yaliyo na nembo ya Airtel Tap Tap hapa nchini, tunaamini huu ni
mwendelezo wa kuboresha mfumo wa uhakika wa malipo kwa teknolojia inayoendana
na sasa” alimaliza kwa kusema Kimea
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Biashara wa Total Nchini, Romee DE VILLENEUVE alisema “Total
tunazaidi ya vituo vya mafuta 30 nchini, hivyo basi tunawahakikishia wateja
wetu wote kupata huduma ya uhakika kila watakapotembelea vituo vyetu vyote na
kununua mafuta au kupata huduma yoyote kwa kutumia kadi hizi za Airtel
Money Tap tap. Tumeona
umuhimu kuboresha mfumo wetu wa malipo kwaajili ya kuwapa wateja urahisi na
usalama zaidi katika vituo vyetu, Tunaishukuru sana Airtel kwa kutuletea
teknolojia hii ya kisasa ya mfumo kufanya malipo kwa kadi ya Airtel Money Tap tap”
Huduma ya
Airtel Money Tap tap imeanza kutumika kwanza jijini Dar es salaam kwa sasa na
baadae itasambazwa nchi nzima katika vituo vyote vya Total.
No comments:
Post a Comment