Mbunge wa jimbo la Mafinga
mjini mkoani Iringa Cosato Chumi akiwa na balozi wa
korea mh Geum-young song wakipata picha ya pamoja baada ya maongezi ya muda mrefu.
na fredy mgunda,iringa
Wananachi wa maeneo
mbalimbali ya jimbo la mafinga mjini wamesema utaratibu wa mbunge wao Cosato
Chumi kwa kwenda kutembelea maeneo yenye kero ni dalili njema zinazoonyesha
kuwa hawakufanya makosa kumchagua kuwa mbunge wao na kuongeza hatadanganywa na
watendaji walioko chini yake tatizo linalosababisha viongozi wengi kutoa
maamuzi yasiyo sahihi na yanayoendelea kuiathiri jamii.
Aidha wananchi hao
wamempongeza mbunge wao kwa juhudi anazo zifanya za kukutana na watadau
mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.
“Tumeona mbunge wetu
akikutana na mabalozi wa nchi tofauti tofauti na wanazungumzia maendeleo ya
jimbo la mafinga mjini mfano hivi karibuni mbunge wetu alikuwa na balozi wa
korea mh Geum-young song tunajua
kunakitu tutapata kutoka kwa balozi huyo”. Walisema wananchi
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mafinga
mjini mkoani Iringa Cosato Chumi ameanza kutimiza ahadi zake
kwa wananchi wa jimbo la Mafinga mjini kwa kufanya
ziara ya kutambua matatizo ya wananchi wake na kutambua nini vipaumbele vyao.
Chumi alisema kuwa lengo la kutimiza
ahadi yake hiyo ni kama njia ya kuwashukuru wana Mafinga
mjini kwa kumchagua katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza
ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa wakati akiomba kura kwa wananchi.
Alisema ataendelea kutimiza
ahadi binafsi zilizotolewa wakati kampeni kulingana na uwezo
wake na zile za kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM
atahakikisha anaikumbusha serikali ya CCM ili kutimiza ahadi
hizo kwa wakati.
“Ndugu zangu wananchi
mbali ya kuwa ubunge wangu ni wa mwaka
mmoja ila tayari mimeanza kutimiza ahadi
bila ya kuchelewa na ninawahakikishieni sita
waangusha nitaendelea kufanya hivyo zaidi
mniombee uzima”.alisema Chumi
Mbunge huyo ameongeza kuwa hivi
karibuni anatarajia kupokea msaada wa kuchimbiwa visima vitano kwenye shule za
sekondari na msingi za jimbo hilo ambapo visima viwili kwa sekondari na vitatu
vya shule ya msingi,msaada huo umetoka kwa ubalozi wa korea mh:Geum-young song.
“Leo nilialikwa lunch na balozi wa
korea mh:Geum-young song na tumeongea mambo mengi lakini kubwa nimeahidiwa
kuchimbiwa visima vitano kwenye shule za msingi na sekondari zilizopo kwenye
jimbo la mafinga mjini mungu ni mwema jambo hili likifanikiwa litatusaidia kuwapunguzia
adha wanafunzi wetu”.alisema Chumi
No comments:
Post a Comment