Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (wa pili kulia)
akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania,
Adriana Lyamba (kulia), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu
kulia), baada ya kuzindua Duka jipya la
Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
- Airtel kufungua maduka mapya Babati, Sumbawanga, Tegeta, Mpanda, Kigoma,
Shinyanga, Singida, Musoma, Songea, na Lindi
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua
duka jipya la kisasa jijini Dar es salaam Mbagala ikiwa ni muendelezo wa
kukamilisha mkakati wake wa kutoa huduma na bidhaa bora za mawasiliano kila mahali
nchini.
Uzinduzi wa duka jipya la Airtel Mbagala uko katika
mkakati waliojiwekea Airtel ambapo hadi sasa wamefanikiwa kujenga maduka mapya 6 katika
mikoa ya Tanga, Moshi, Kariakoo, Kahama, Mwanza ndani ya Rock City Mall pamoja
na duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel Moroko jijini
DSM. Sambamba na hilo Airtel imekarabati maduka yake yote nchini ili kutoa
huduma zinazoendana na karne ya sasa katika sekta ya mawasiliano.
Akizindua hilo Mbagala jijini Dar es salaam
Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi Sophia Mjema aliipongeza Airtel na kuwataka wakazi
wa Mbagala na maeneo ya jirani kulitumia vyema duka hilo katika kupata huduma
za mawasiliano kwa kuwa mawasiliano sasa yanachangia sana katika maendeleo ya
jamii.
“Ninawapongeza sana Airtel kwa ha kufungua
duka hapa MBAGALA, ninatambua huduma ya mawasiliano ni chachu ya maendeleo ya
jamii na nchi kwa ujumla, tunajionea jinsi baadhi ya huduma za kimtandao kama
Airtel Money zilivyo na usalama kwa jinsi zinavyowawezesha watumiaji hata
kutunza pesa zao, kulipia ankara mbalimbali, kutuma na kupokea pesa pamoja na
kujipatia mikopo kama ilivyo huduma ya kipekee ya mikopo isiyo na masharti
ijulikanayo kama Airtel TIMIZA sasa”.
“Nitoe wito sasa kwa wakazi wa MBAGALA, sasa
tumieni duka lenu hili la karibu kujipatia huduma mbalimbali, kusajili namba za
simu pamoja na kuzihakiki ili kutimiza maagizo ya serikali ya kwamba kila
anaetumia namba ya simu iwe imesajliliwa kwa jina lake ili kupunguza uhalifu”.
|
No comments:
Post a Comment