Skauti wa TZ na wengine wa nchi
za Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani Arusha. |
Skauti Tz na wengine kutoka nchi za
afrika mashariki
wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi
rasmi wa kambi ya
mashindano inayoendelea mkoani
Arusha
Skauti kutoka Kenya na
wengine wa nchi za Afrika Mashariki
wakipita mbele ya mgeni
rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya
mashindano ya skauti nchi
za afrika mashariki inayoendelea mkoani
Arusha.
Na Woinde Shizza,Arusha
Vyama vya scout kanda ya Afrika Mashariki
vimekutana mjini hapa kuanza
mashindano ya mascout
yenye lengo la kuwezesha vikosi vya scout
kushindana pamoja ili
kujipima katika utekelezaji wa programu ya vijana ya
stadi za
kiscout katika vikosi na jumuiya ya afrika mashariki ambazo
wamekuwa wakijifunza katika maeneo yao.
Akizungumza katika
mashindano hayo yalioanza jana meneo ya kisongo jijini
hapa,kamishna mkuu wa chama cha skauti tanzania Rashidi Mchata alisema
kuwa mashindano hayo yameshirikisha vijana wa kiscout
kutoka nchi tano za
Jumuiya ya afrika mashariki.
Mchata alisema kuwa mashindano hayo yatahusisha makundi ya mascout
wadogo, mascout wakubwa na masouti vijana kutoka kila nchi
yatashindana
kutengeneza stadi za kiskauti kwa kutumia mbinu zao
ambazo wamekuwa
wakifundishwa katika vikosi vyao kwa
ajili ya kuwawezesha kuhudumia jamii
na kuwafanya wawe
wazalendo.
"Vyama vya mascout kutoka jumuiya ya afrika
tumekutana hapa arusha kwa
malengo matatu ikiwemo mashindano
,jukwaa la vijana mascout lakini pia
tumekuwa na mkutano mkuu wa
makamishna wa skauti kutoka nchi za jumuiya na hii inasaidia kwa
pamoja kuhakikisha kuwa vijana wetu wanakuwa wazalendo na kupitia haya mashindano tutaweza kuwapata washindi ambao wanawakilisha
nchi zao walizotokea"alisema Mchata.
Rehema
Ramadhani mwanascout kutoka dar es salaam ambae anawakilisha
tanzania katika mashindano hayo alisema kuwa mashindano hayo
yanajumuisha mambo yote waliokuwa wanafundishwa kuanzia ngazi ya
wilaya na kwamba yanawapa uzoefu wa stadi zao kutoka kwa mascout
wa nchi nyingine za jumuiya ya afrika mashariki.
Alisema kuwa katika vikosi vyao wamekuwa wakifundishwa mambo mbali
mbali ikiwemo utunzaji wa mazingira kama ilivyo kauli mbiu ya
rais magufuli
lakini pia jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu
au jamii pale inapopata
janga na hivyo wanaamini kuwa
wataiwakilisha tanzania kuwa mshindi katika
mashindano
Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la vijana wa kiscout
katika jumuiya
ya afrika mashariki Murtadhwa Abdallah alisema
kuwa taasisi mbali mbali
zinatakiwa kujitokeza na kushirikiana
katika kufadhili scout kwani vyama
hivyo vimekuwa vikikabikiwa
na changamoto ya fedha hivyo kushindwa
kujiendesha
vyenyewe.
No comments:
Post a Comment