Suleiman Msuya
IKIWA ni takribani miezi
10 sasa kwa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif
Hamad kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Bugurunina kundi la Profesa Ibrahim
Lipumba chama hicho kimezindua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa,
Kata ya Mzimuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aidha,
Seif amesisitiza kuwa hatarajii kukutana na Profesa Lipumba kwa kile alichodai kuwa hatambuliki katika chama na hana sifa hizo kwa sasa.
Akizindua ofisi hiyo ambayo lengo kubwa ni kwa ajili ya wabunge
40 wa CUF, Seif alisema uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni cha
kiungwana na kinahitajika kuungwa mkono na wanachama wote.
Alisema kwa muda wa miezi
10 sasa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi hasa upande wa Tanzania Bara
jambo ambalo limewaathiri sana hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu yake vilivyo bila hofu yoyote.
Maalim Seif alisema kukosa ofisi kumewaathiri sana katika baadhi ya
mambo hivyo anaamini kwa sasa akifikia Dar es Salaam anamahali pa
kukutana na wakurugenzi wake.
“Nimekuwa ni kija hapa nakosa sehemu ya kukutana na wakurugenzi,
viongozi mbalimbali wanachama ila hiki ambacho wabunge wamefanya ni cha
kuungwa mkono sijawahi kufanya kazi na wabunge wanao kipenda chama kama kipindi hiki,”
alisema.
Katibu huyo alisema atahakikisha kuwa anaanza kazi haraka iwezekanavyo kwa kukutana na wakurugenzi
wake ili waweze kutekeleza majukumu ya chama.
“Hakuna shaka kuwa hu u unaoitwa mgogoro umeturudisha nyuma sana hivyo naamini wakati wa kufanyakazi umerejea na hawa wabaya wetu hawata ambulia kitu kwani
CUF ni chama imara hakitikisiki,” alisema.
Maalim Seif alisema jitihada zinazofanywa na
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimaliza chama ni kubwa lakini hawataweza kufikia lengo hilo kutokana na misingi ya chama hicho.
Alisema kwa sasaa atafanya kazi katika ofisi hiyo ambayo amepewa na wabunge hadi hapo muafaka wa ofisi kuu Buguruni utakapopatikana huku akisisitiza kuwa haki haipotei ila inachelewa.
Katibu huyo alisema anaimani na mahakama kuwa ita wapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.
Aidha,
alisema kupitia mgogoro huo hadi sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inashikilia zaidi ya
sh. bilioni 1.2 ambazo ni ruzuku ya chamahicho.
Maalim Seif alisema fedha hizo ni pamoja na zile ambazo ofisi ya msajili ilimpatia Lipumba hivyo waamini mgogoro ukiisha wata pata haki yao.
Kwa upande mwingine Katibu huyo alisema hana mpango wa kukutana naLipumba kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kuwa si kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.
Alisema CUF haimtambui Lipumba kwa sifa yoyote tofauti na kumfukuza uanachama hivyo yeye hawezi kukukutana na mtu kamahuyo.
Maalim Seif alisema pamoja na kuwa hawamtambui Lipumba kama kiongozi
au mwanachama ila akiomba msamaha wapo tayari kumsamehe.
Akizungumza baada ya kuzinduliwa ofisi hizo Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa Wabunge wa
CUF bungeni,
Riziki Ngwali alisema wamelazimika kufungua ofisi nyingine ili wapate mahali pa
kukutana wakiwa nje ya Bunge.
Ngwali alisema kupitia ofisi hiyo wataweza kujadiliana
mambo mbalimbali yanayo wahusu wabunge na wananchi na kuja na ufumbuzi.
Kwa upande wake
Mbunge wa Temeke CUF,
Abdallah Mtolea alisema katika ofisi hiyo wanatarajia kuajiri wataalam mbalimbali ambao watasaidia kufanya tafiti na kupitia tarifa mbalimbali za
Bunge ili kuwarahisishia katika uchangiaji bungeni.
Alisema katika ofisi hizo wameingia mkataba wa kulipa
sh. milioni 18 kwa mwaka ambazo zitatolewa na wabunge wenyewe kwa maslahi ya chama chao.
No comments:
Post a Comment