MKUU wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo akifungua semina ya siku mbili ya fursa mpya ya kuongeza mapato ya
halmashauri nchini kwa wakurugenzi wa majiji na manispaa iliyoandaliwa na
shirika la maendeleo la UNCDF iliyofanyika jijini Arusha jana.
Mratibu wa mfuko wa mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Peter Malika
akizungumza
Mratibu wa mfuko wa mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Peter Malika
akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo na kusema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa
majiji matato na manispaa tatu.
Baadhi ya wakuregenzi wa majiji na Manispaa waliohudhuria
SHIRIIKA la maendeleo ya mitaji la umoja wa Mataifa(UNCDF), jana limezindua
mpango wa kuziwezesha halmashauri za majiji na Manispaa kuweza kunufaika na
masoko ya mitaji kwa kuwekeza katika soko la la hisa kuuza vipande na
kutoa hati za dhamana.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alizindua mpango huo jijini hapa kwa niaba ya
Waziri wa nchi ofisi za Rais(TAMISEMI) George Simbachawene na kuwataka
watendaji na halmashauri za majiji na manispaa ,wanaohudhuria mafunzo hayo
kujiandaa kutumia fursa hiyo.
Gambo
alisema katika mpango huo, ambao unatarajiwa kuongeza mapato kwa halmashauri za
majiji na manispaa nchini, kutokana na kuelimisha ni jinsi gani wataweza
kuwekeza katika soko la hisa na kupata fedha za miradi ya maendeleo.
Alisema
mpango huo, ambao unataribiwa na UNCDF unaziezesha halmashauri kupata fedha
nyingi ambazo zitawezesha kuendesha miradi mikubwa ya miundombinu na hivyo
kuchochea wanannchi.
Awali,
Mratibu wa mfuko wa mitaji wa umoja wa mataifa(UNCDF) Peter Malika
alisema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa
majiji matato na manispaa tatu.
Malika
alisema Majiji ambayo yatakuwa katika mpango huo ni Dar es Salaam,Mwanza,
Arusha, Mbeya na Tanga na Manispaa ambazo zitahusika ni
Kinondoni,Temeke,Ilemela na Dodoma.
"Majiji
haya na manispaa wanauwezo wa kuanza kuwekeza katika masoko ya hisa kwa kuuza
hati za dhamana na wataweza kupata fedha kwa miradi mikubwa ya
maendeleo"alisema.
Mkurugenzi
wa jiji la Arusha, Athuman Kihamia, alisema mpango huo tayari umeonesha
mafanikio katika majiji kadhaa, ikiwepo Afrika Kusini, Marekani na Asia
na wanatarajiwa utaboresha mapato ya halmashauri.
Kihamia
alisema jiji la Arusha tayari limejiandaa kunufaika na mpango huo na tayari
lina kampuni ya Arusha Investment ambayo inaweza kushiriki katika masoko ya
hisa.
No comments:
Post a Comment