Tangazo

September 28, 2011

AIRTEL TANZANIA NA ENGEN PETROLEUM ZACHANGIA KUFANIKISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (kulia) akikabidhi stika hizo kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hii leo. Wengine ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaaban Kayungilo na Mjumbe wa barazala Taifa la Usalama Barabarani Henry Bantu. (Picha na Mpigapicha wetu)
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaban Kayungilo na (katikati) ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika hizo kwa waandishi wa habari. (Picha na Mpigapicha wetu)
Kamishna Mohamed Mpinga akionesha stika hizo za aina tatu kwaajili ya magari, pikipiki na bajaji ambazo mwaka huu zinaalama maalum ambazo haziwezi kufojiwa kirahisi.
Meneja Masoko waKampuni ya Mafuta ya Engen, Shaaban Kayungilo (kulia), akikabidhi stika hizo kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hii leo. Wengine ni Mkuu waMawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano  Mallya na Mjumbe wa barazala Taifa la Usalama Barabarani Henry Bantu. (Picha na Mpigapicha wetu).
                                    **************************************************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta ENGEN kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia baraza la taifa la  usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti namba ya ajali za barabarani nchini.

 Leo tumekutana hapa kutangaza wiki ya nenda kwa usalama ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo  huko mkoani Bukoba. ENGEN Tanzania kampuni ya nishati ya magari nchini Tanzania na Airtel kampuni ya mawasiliano zilikubaliana kuungana na serikali kupitia Baraza la Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kuhamasisha jamii kahusu usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ENGEN Meneja Bidhaa Jacqueline Kisoka Kupitia SLOGAN ya mwaka huu inayosema “ Usalama barabarani unahitaji uwajibikaji wa kila mtu” ENGEN Tanzania inayofuraha kuwa sehemu ya jitihada za kuokoa  maisha ya watu katika jamii yetu na imejitoa kuhamasisha jamii nzima kuzingatia usalama barabarani kama mchango wake katika huduma kwa jamii. ENGEN ni sehemu ya watumia barabara na watumia barabara wengi hutumia bidhaa za ENGEN ndio maana ni mategemeo ya  ENGEN kuwa watumia barabara wote wawe salama ili iweze kuwahudumia.

 Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kwa miaka 3 mfululizo Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama Barabaaarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa. Mchango wetu kwa mwaka huu ni kuchapisha stika na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo  T shirt 2,200 zenye ujumbe  wa mwaka huu “Usalama Barabarani unahitaji juhudi za kila moja wetu” .

Matokeo ya ajali za barabarani ni moja ya masuala muhimu kiafya kitaifa. Kila mtumia barabara anahusika awe mwendesha gari, pikipiki au mtembea kwa miguu. Kila mwaka maelfu ya wanaume, wanawake na watoto hufariki kutokana na ajali za barabarani hivyo kusababisha upungufu wa nguvu kazi katika shughuli za uzalishaji kiuchumi. Hii ndio sababu Airtel imejiingiza katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha jitihada hizi”.

Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza.

 

No comments: