Tangazo

September 27, 2011

BALOZI WA BRAZIL NCHINI, FRANCISCO LUZ ATOA USHAURI WA KUWAWEZESHA WATANZANIA KUISHI MAISHA BORA

Balozi wa Brazil nchini Tanzania Bw. Fransisco Luz
Na Mwandishi wetu

Balozi wa Brazil nchini Tanzania Bw. Fransisco Luz amesema, Serikali ya Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi kwa upana wake ila inahitajika  kufanya kazi ya ziada kuhakikisha inatengeneza  nafasi nyingi za rasilimali watu ambalo ndilo tatizo kubwa linalopelekea nchi kuyumba kiuchumi na wananchi wake wengi kuendelea kuwa maskini.
 
Balozi Huyo aliyasema hayo katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye ofisi za Balozi huyo zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es salaam, wakati  mwandishi wa habari hii alipotaka kufahamu maandalizi ya ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda , anayetarajiwa kufanya ziara ya siku Sita nchini Brazil kuanzia mwanzoni mwa Mwezi ujao.
 
Balozi LUZ alisema, Kutokana na nchi ya Tanzania kuwa na Rasilimali nyingi akitolea mfano GESI ya ASILI,Makaa ya Mawe na Mafuta  ambayo yako katika mchakato wa kutafutwa kupitia  kampuni kutoka nchini Brazil,  katika maeneo ya bahari ya hindi, Tanzania itaweza kufanikiwa kwa  kiwango cha juu katika kukuza  uchumi wake pamoja na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo ambao ndiyo wainua uchumi wa nchi.
 
Amesema, Nchi nyingi  zilizoendelea  hivi karibuni zmeionyesha nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania  kutokana na ukweli kuwa kuna nafasi nyingi za kufanya hivyo katika maeneo ya Nishati, lakini kinachokwamisha ni suala la NISHATI na Miundo mbinu ambalo limekuwa ndiyo changamoto kubwa katika kuwezesha hilo na limeendelea kukua siku hadi siku.
 
Aidha Balozi LUZ akizungumzia nchi yake ya Brazil ambayo awali ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la kiuchumi na sasa kuibuka kuwa Taifa linaloibukia kiuchumi pamoja na nchi za BRICS,Alisema kuwa, Awali kila kitu kilikuwa mikononi mwa serikali na hivyo kusababisha mambo mengi kutoenda sawa lakini baadaye wapenda maendeleo walikaa na kuamua kuweka mpango uliwezesha kuwainua watu wa daraja la kati ambao ni wengi kwa kuwapatia msaada wa pesa na kuwasaidia familia maskini .
 
Akizungumzia suala la Rasilimali watu, aliishauri Serikali kuanzisha vyuo  AU Kushirikiana na vyuo vikuu vitakavyotoa elimu ya juu katika kuwezesha kutoa  wahitimu wenye sifa za kufanya kazi katika sekta za Nishati akitolea mfano shughuli itakayohitaji wahandisi wengi wa uchimbaji mafuta katika kipindi kijacho.
 
Kuhusu Safari ya Mheshimiwa waziri Mkuu,Balozi LUZ amesema, Katika ziara hiyo mheshimiwa waziri anatarajiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kuvutia na yatakayoleta tija kwa nchi ya Tanzania, zikiwemo sekta za kilimo kwasababu kilimo Kwanza ndiyo kipaumbele cha nchi, pia atatembelea maeneo ya mifugo, Miundombinu  pamoja na miradi ya mbalimbali ya maendeleo nchini humo sambamba na kukutana na wafanyabishara wenye nia ya kuwekeza Tanzania na muungano wa vyama mbalimbali.
 
Sambamba na hilo balozi huyo wa Brazil amesema, Waziri Mkuu pia katika ziara hiyo  atakutana na Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi ya Brazil pamoja na mawaziri wengine.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu PINDA , ataongozana na msafara wa Viongozi kadhaa kutoka hapa nchini Akiwemo waziri wa Nishati na Madini Bw.William Ngeleja, Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu pamoja na viongozi wengine wa juu wa serikali .

Habari na Picha kwa Hisani ya Zainul Mzige wa MO BLOG

No comments: