Tangazo

September 14, 2011

Ibra Kaude wa Vodacom apata 'Stove'

Mwenzagu Pokea pete hii iwe ishara ya upendo wangu kwako na uaminifu wangu kwao. Ndivyo inavyoonekana Rahma akisema wakati alipokuwa akimvisha pete ya ndoa mme wake Ibra Kaude wakati wa harusi yao iliyofungwa Ijumaa ya Septemba 9 mwaka huu katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe Mkoani Morogoro. Sherehe ya kuwapongeza ilifanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Jumapili ya Septemba 11. Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania. (Picha zote na Albart Jackson) 
Ibra Kaude na mke wake Rahma Othumani Mohammed wakiwa katika pozi la picha wakati wa sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Hayawi hayawi yamekuwa ilikuwa siku wiki,mwezi,miezi miaka, hadi sikumikatimia Maharusi Ibra Kaude akiwa na mkewe Rahma Othumani Mohammed wakionyesha shahada za vyeti vya Ndoa baada ya kufunga ndoa yao katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe Mkoani Morogoro.
Bwanaharusi Ibra  Kaude na Rahma Othumani Mohammed, wakiwa katika pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao.
Kaka wa bibi harusi Rahma Othumani ,Hifidh Othumani akimfungisha ndoa Ibra Kaude (kulia ) huku wakiongozwa na sheikhe kutoka Bakwata jijini Dar es Salaam.
Bwana harusi Ibra Kaude akisaini cheti cha ndoa baada ya kumaliza swala ya ndoa katika msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe Mkoani Morogoro.

No comments: