Tangazo

October 7, 2011

TBL YAKABIDHI MRADI WA MAJI WA 21,000,000/- KATIKA SOKO LA MACHINGA MCHIKICHINI

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia), Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu wakiwa na furaha wakati wa hafla ya kukabidhi mradi huo wa maji kwa uongozi wa Soko la Machinga la Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia), akihutubia wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto), akishikana mkono na Mwenyekiti wa Soko la Machinga Mchikichini,  Deo Mkali ikiwa ni ishara ya kukabidhi mradi wa maji wa soko hilo, Dar es Salaam jana,, uliojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa gharama ya sh. milioni 21 . Katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Machnga la Mchikichini, wakiteka maji baada ya mradi huo uliojengwa kwa msaada wa TBL, kwa sh. mil. 21, kukabidhiwa kwa uongozi wa soko hilo leo.
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu (kulia) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akifungulia maji  wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambao ulikabidhiwa kwa uongozi wa Soko la Machinga. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo ambayo imejenga mradi huo kwa sh. mil. 21.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akimtwisha mfanyabiashara wa Soko la Machinga la Mchikichini, Asumpta Mosha ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa kwa sh. mil. 21 na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Hafla hiyo ilifanyika sokoni hapo Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo akisaidia kumtwisha mfanyabiashara wa Soko la Machinga la Mchikichini, Asumpta Mosha ndoo ya maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa kwa sh. mil. 21 na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Hafla hiyo ilifanyika sokoni hapo Dar es Salaam leo. Picha na Richard Mwaikenda

No comments: