Tangazo

October 6, 2011

Mlemavu asaidiwa 800,000/= ili akajiunge na Shahada ya Uchumi Mwalimu Nyerere Memorial Academy

Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd, Bi. Joyce Shebe akiwa ameshikilia kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema tayari kumkabidhi Mlemavu Frida Kavishe kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi  katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Kutoka Kulia ni kaka wa Frida, Omari Mkete na Mhariri wa Habari Clouds FM/TV Bw Lazaro Matarange.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd,  Bi. Joyce Shebe akimkabidhi  kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema kwa Mlemavu Frida Kavishe alizoomba kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi  katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Anayeshuhudia ni kaka wa Frida, Omari Mkete.
Bi Frida Kavishe mlemavu anayetarajia kujiunga na Shahada ya Uchumi  katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akiwa na kaka yake Omari Mkete nje ya Ofisi za Clouds Media Group Ltd baada ya kupokea msaada wa fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema ili akalipie ada.Picha na Jerome Risasi

No comments: