Tangazo

October 7, 2011

ASHIKILIWA NA POLISI MKOANI MBEYA KWA KUMSHINIKIZA MKEWE KUNYWA SUMU HADI KUFA

Mtuhumiwa Bwana Mohamed Mwawipa ambaye alimshinikiza mkewe Nuru Masuba kunywa sumu baada ya kumtuhumu kuwa amemwibia fedha taslimu 450,000/- akionesha askari wa upelelezi eneo alilonywea sumu mkewe.
Mweyekiti wa kijiji cha Ijumbi Kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali, Bw. John Mkalimoyo akimfariji dada wa marehemu Nuru Masuba aitwaye Stumai Wilson ambapo marehemu alikuwa akiishi naye Kijiji cha Mapogolo Kapunga.
Mwili wa marehemu Nuru Masuba ukipelekwa kuhifadhiwa kaburini, baada ya uchunguzi wa daktari na polisi kukamilika. Picha & Habari na- Mbeya Yetu Blog 
                                                        XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na mwandishi wetu
Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ameshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.

Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asigekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipoulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali.
 
 
 

No comments: