Tangazo

January 17, 2012

Airtel yazindua rasmi huduma ya kununua mafuta ya gari kwa Airtel Money katika vituo vya Gapco

Mteja wa Airtel money Bw David Ramadhani akitumia simu yake ya Airtel kununua mafuta ya gari kwa kutumia huduma ya Airtel money katika kituo cha Gapco jijini Dar-es-salaam. Anaemuwekea mafuta ni muhudumu wa kituo hicho Bi. Nina Owiso  na wa kwanza kushoto ni Mercy Nyange Afisa Uendeshaji wa Airtel Money akishuhudia mara baada ya hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ya  kununua mafuta kwa kutumia Airtel Money katika vituo vya Gapco Dar es salaam iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Meneja uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Bw Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya kununua mafuta ya gari na ya taa kupitia huduma salama,rahisi na ya haraka ya Airtel money jijini Dar-es-salaam jinsi wanavyoweza kufaidika na huduma hiyo ambayo itawarahisishia maisha ya kila siku kuepuka kutembea na pesa nyingi mifukoni lakini wakiwa na huduma hiyo wanaweza kuepuka usumbufu huo . uzinduzi rasmi wa kununua mafuta kwa kutumia Airtel Money katika vituo vya Gapco Dar es salaam umefanyika mwishoni mwa wiki.    
                        ************************************************************
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kuvitangaza vituo vitakavyotoa huduma hio kwa sasa jijini Dar es salaam, Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando  alisema " Lengo letu Airtel kupitia Airtel Money ni kuhakikisha huduma hii ya Airtel Money inakuwa suluhisho la kudumu kwa
mahitaji ya kila siku kwa wananchi wote na wateja wetu kwa ujumla.

Sasa unaweza kupata huduma katika vituo vya Gapco Dar es salaam pale Sasa kazi-Mtoni Mtongani, Gapco Banana-Gongo la Mboto, na Gapco-bara bara ya Samora Lengo letu baada ya miezi miwili ijayo tuwe tumesambaza huduma hii ya
kununua mafuta kwa Airtel Money katika kwa vituo vingi zaidi na watoa huduma hii wote! Aliongeza kusema Mmbando.

Mbali na kutoa huduma ya kununua Mafuta kwa Airtel money vituo hivi pia ni Wakala wetu ambao pia mteja ataweza kutoa au kutuma fedha wakati wote vituo hivi vinapokuwa wazi

Meneja Mauzo wa GAPCO, Mr Ben Temu alisema "huduma ya kununa mafuta ni rahisi kupitia Airtel Money, Wateja wote wa Airtel tunawakaribisha katika vituo vyetu vya Sasakazi- mtoni mtongani, banana-Gongo la Mboto na kile cha Bara bara ya samora mjinunulie mafuta kwa kupitia Airtel
Money

Aaliongeza kwa kusema " Ninaipongeza sana Airtel kwa kuja na huduma hizi bora zinazoonyesha ubunifu wa hali ya juu sasa hii inatupunguzia hatari ya kutembea na kiasi kikubwa cha pesa kadhalika hata wamiliki au wafanyabiashara wa petrol na disel kama sisi" alisema Mr Temu.

No comments: