Tangazo

January 17, 2012

ZANTEL YATEUA MKURUGENZI MPYA WA MASOKO

Brian Karokola
Zantel ambayo ni kampuni Tanzu ya ya Etisalat Group  na ambayo ni kampuni ya simu selula yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania  inayofuraha kutangaza kuwa  imemteua Bw. Brian Karokola  kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Masoko pamoja na Bw. Deo Kwivukwa  kuwa Mkuu wa Idara ya Usambazaji na Mauzo kuanzia Januari 02, 2012.

 Jukumu jipya la Bw. Karokola  kama Mkurugenzi wa Masoko  litakuwa ni kusimamia programu ya mikakati ya mipango ya  masoko, mawasiliano ya kampuni kwa kuangalia  mtiririko wa mapato ya rejareja  na kubuni mipango mipya. Nafasi hiyo ni muhimu katika kuendelea  kukua kwa bidhaa za Zantel  pamoja na  soko  lake nchini Tanzania.
  
Ofisa Mkuu wa biashara wa Zantel, Ahmed Mokhles akiidhinisha  uteuzi huo alisema kwamba Zantel ni mwajiri wa kuchaguliwa na Watanzania  na chimbuko la kukuza utaalamu  wa ndani. 

“Ninayo furaha kuwatangaza uteuzi wa Bw. Karokola  kama Mkurugenzi wa Masoko na kuifanya Zantel  kuongoza  miongoni mwa waendeshaji wa  mitandao ya simu selula kwa kuteua mzawa kuongoza kitengo chake cha masoko. Hili lipo kwenye majukumu ya Etisalat Group katika kuwekeza kwenye wataalamu wa ndani”, alisema Mokhles.

Brian Karokola ana Shahada  ya Uzamili kwenye Masoko (MBA) na hivi karibuni alimaliza  programu ya miezi 12 ya HiPo ambayo inajumuisha programu ya uongozi kibiashara kazini  kwenye mawasiliano ya simu inayotolewa kwa ubia  kati ya Etisalat Academy  kwenye Falme za Kiarabu (UAE) na Skuli ya Biashara ya Harvard ya  Marekani   


Deo Kwivukwa kwa upande wake kama Mkuu wa Kitengo na mauzo  jukumu lake litakuwa ni kuangalia  usambazaji, timu ya mauzo  na kusimamia mwenendo wa usambazaji  nchini hali kadhalika kuwezesha na kupanua bidhaa za Zantel zisambae nchini kote. Kabla ya uteuzi wake  alikuwa ni  msimamizi wa kitengo cha Zantel Own Manager  kinachoshughulikia maduka na  vituo vya huduma kwa  wateja . ana Shahada ya Uzamili kwenye  Masoko  akiwa amejikita kwenye  masuala yanayoliweka soko kwenye hali mbaya (MBA venturing in Marketing) .


Kuhusu Zantel:
 Zantel ani jina rasmi  la biashara la Kampuni ya simu ya Zanzibar Telecom Limited. Ikiwa ni kampuni ya nne  inayotoa huduma ya simu selula  nchini Tanzania. Zantel  ni kampuni ya Kitanznaia  iliyojikita kwenye  kuimarisha maisha ya wateja wake  kupitia mawasiliano yaliyoboreshwa. Kwa kutoka huduma yenye thamani, ubora wa hali ya juu  na huduma nzuri Zantel inataka kuwapa wateja wake  huduma  zitakazowafanya  waziamini iwe ni kwenye kuendesha biashara  kwa ufanisi au  kuwasiliana na marafiki na familia.

Hudfuma zinazotolewa na Zantel ni pamoja na  huduama ya mawasiliano ya simu za kufunga  na zisizo za waya huduma za kimataifa za  kupeleka na kupokea , huduma za mawasiliano za takwimu na intaneti CDMA, IP telephony na VOIP na Mtandao wa huduma ulioongezwa thamani (VANS).

 Zantel ni kampuni ya kwanza  binafsi  nchini Tanzania  kumiliki  lango la kimataifa  ambalo limeiwezesha  kupunguza kiwango cha  miito ya simu kimataifa  kwa asilimia 60  hivyo kufungua mlango wa upigaji simu rahisi kimataifa ndani ya nchi. Zantel inatoa viwango ambavyo wateja wanavimudu  na vilivyo vya ushindani kimataifa nchi kwenda maeneo yote maarufu  kimataifa duniani  na inashirikiana na kampuni nyingi za simu selula kuhakikisha kuwa wateja wanatumia Zantel  sehemu yoyote duniani.

Leo hii mtandao wa Zantel  unapatikana katika majiji yote na miji yote mikubwa, barabara kuu na maeneo ya vijijini ya Tanzania.




No comments: