Tangazo

January 23, 2012

GAPCO Tanzania yadhamini Walemavu katika Kilimanjaro Marathon 2012

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu udhamni wa kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya Gapco Tanzania wa mbio za Nusu Marathoni kwa watu wenye ulemavu zikiwa ni sehemu ya Mbio za Kilimanjaro Marathon 2012 zitakazofanyika februari 26 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mwakilishi wa Hoteli ya Sourthern Sun ambayo ni miongoni mwa wadhamini, Bi. Judith Muya, Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Gapco Tanzania, Ben Temu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wild Frontiers waandaaji wa mashindano hayo, John Addison (kulua). Picha Zote/ Daily Mitikasi Blog

Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Gapco Tanzania, Ben Temu akifafanua jambo kuhusu udhamini wa kampuni yake.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui na  Mwakilishi wa Hoteli ya Sourthern Sun, Bi. Judith Muya wakifurahia jambo kabla ya kuanza mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya Southern Sun iliyopo katika Mtaa wa Garden jijini.

Mkutano ukiendelea.


No comments: