Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM ambayo yataanza mwanzoni mwa mwezi Februari na kufikia kilele chake Februari 5, 2012.PICHA/BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema maadhimisho ya kuzaliwa kwake ya mwaka huu pamoja na mambo mengine kitayatumia kupiga vita wagombea wote wanaotoa na kupokea rushwa wakati wake mkuu.
Pia kitatumia maadhimisho hayo kuhamasisha wananchama wake waadilifu na waaminifu kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika mwaka huu, kuanzia ngazi za mashina hadi taifa.
Hayo yalisemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.
Nape alisema, Chama kitatumia fursa hiyo pia kuwaelimisha wanachama wake na wananchi kwa jumla kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi yanayokusudiwa kufanyika, ikiwa ni pamoja na msimamo wa kuilinda nchi, amani, na kupatikana kwa Katiba bora itakayokuwa na manufaa kwa watu wote.
Alisema, maadhimisho hayo yataanza Februari mosi na kufikia kilele chake Februari 5, 2012 yakiambatana na shughuli mbalimbali yakiwemo matembezi ya mshikamano yatakayofanyika kila mkoa wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo kitakachofanyika Mwanza.
Nape alisema ..................
"Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi kufikisha miaka 35 ya uhai wake yangu vyama vya TANU na ASP vilipovunjwa na kuundwa chama kipya cha CCM chenye nguvu, Februari 5, 1977",lisema Nape na kuongeza.
"Sherehe hizo huadhimishwa kwa Chama na Jumuia zake kufanya shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii. Aidha, Kitaifa Chama huteua mkoa mwenyeji wa sherehe hizi ambazo huambatana na matembezi ya mshikamano".
Alisema kwa kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu wa Chama kimependekeza kaulimbiu mahsusi itakayotumika katika sherehe hizo kuwa ni "CCM Imara na Madhubuti inaanza na mimi; naimarisha Chama Changu kwa kuchagua viongozi bora na waadilifu".
Nape alisema uzinduzi wa sherehe hizo utafanyika kila mkoa Januari 30, mwaka huu na kufuatiwa na wiki ya shughuli za Jumuia, ambazo kila Jumuia itapanga ratiba ya mikutano ya ndani na shughuli za kijamii kama kupanda miti.
CCM imewataka wajumbe wa Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya mikoa kutumia wiki hiyo kufanya ziara katika matawi kuimarisha uhai wa Chama. |
No comments:
Post a Comment