Tangazo

January 18, 2012

Rais Kikwete azindua madaraja makubwa mawili Morogoro Vijijini, aweka Jiwe la Msingi la Soko na kuhutubia katika mvua kubwa

Rais Jakaya Kikwete akielekea jukwaani kuhutubia wananchi  baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa soko la kijiji cha Mtamba, Morogoro Vijijini. Rais Jakaya Kikwete jana ametembelea Morogoro Vijijini na kuzindua madaraja mawili makubwa katika Mto Mtombozi, Matombo na Mto Magogoni katika Barabara ya Kiganila - Mvuha, pia ameweka jiwe la msingi la Soko la Kijiji cha Mtamba na kukagua ujenzi wa barabara sehemu ya Kisaki, Msalabani. PICHA ZOTE NA IKULU

JK akiongea baada ya kuzindua daraja la mto Mtombozi tarafa ya Matombo wilaya ya Morogoro mjini leo January 17, 2012

JK na RC Joel Bendera wakivuka daraja jipya la Magogoni katika barabara ya Kiganila-Mvuha, Morogoro Vijijini baada ya kulizindua

JK na ujumbe wake na wenyeji wakipita juu ya daraja jipya la  Mtombozi, Matombo, Morogoro vijijini alilozindua.


No comments: