Tangazo

March 7, 2012

Licha ya Kutangazwa Mgomo wa Madaktari: Hospitali ya Mwananyamala waendelea Kudunda Mzigo kama kawaida

Dk. Minja wa Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam  akichukua maelezo kutoka kwa Zulfa Rashid ambaye anaelezea jinsi mtoto wake Warida Juma anavyoumwa. Wafanyakazi wa Hospitali hiyo wanatimiza maadili yao ya kazi kwa kutoa huduma kwa wagonjwa licha ya kutangazwa kwa mgomo wa madaktari wa Hospitali za Serikali ulioanza leo hapa nchini.

Muuguzi  wa Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam Christer Senihyina akisoma vyeti vya mgonjwa ili aweze kumpatia dawa Tatu Omari  aliyefika hospitalini hapo kwa ajili ya kumchukulia mtoto wake dawa.

Dk. Erasmina Maina akimuelekeza Gola Abdala (kushoto) ambaye ni kaka wa mgonjwa Abdala Saidi jinsi ya kwenda kutumia dawa mara baada ya kupata matibabu katika  Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam  kulia ni muuguzi Meckitrida Mashauri.

Wagonjwa katika  Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kwenda kupigwa Utra Sound kama walivyokutwa na kamera yetu.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments: