Tangazo

March 8, 2012

HOJA YA HAJA: MGOMO WA MADAKTARI

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Nkopi
Habari Ankal Michuzi na Wanalibeneke woote,

Ni Tumaini langu kuwa mu Wazima,samahani sana kutumia Neno hili lakini Nadhani Mnachokifanya ni UKATILI,USALITI na Kuwapiga Mateke Watanzania Ambao Kodi zao ndio zimekupeni TAALUMA hiyo ambayo mnatumia Sasa Kwa MAKSUDI kuwaua Watanzania.

Katika Majadiliano yoyote Huwezi Kuingia na Kutaka YAKO TU ndio Yachukuliwe Kama ni hivyo Hakuna HAJA YA MAJADILIANO,ukiingia na RIGIDITY kuwa Yangu yote Yatimizwe huna haja ya kujadiliana basi na Huna NIA YA SULUHU,ukikubali Majadiliano Lazima ukubali kuwa FLEXIBLE Ukubali WIN-win Situation ,You win a little and Loose a little,hiyo ndio Formula ya kufikia Maafikiano ktk Majadiliano yoyote.

Hivi tukijenga Precedent ya Watu kutumia Umuhimu wao KUBLACKMAIL serikali Nchi Hii Itakwenda wapi?? Wataalam wanaojua Mfano kuendesha Mitambo ya Umeme,Maji Wote wakiamua izimwe ili Matakwa yao yatimizwe??

Ninyi hizo Mashine Mtazitumia??,Wanajeshi wanaolinda Mipaka yetu Maporini Mvua,Radi Zao?? Polisi?? Nk itakuwaje? Sisi ni kama Mwili wa Binadamu kila Kada kwa Nafasi yake inao Umuhimu wake, ni Majukumu Yanapishana tu,Kuwa Daktari Anaokoa Maisha ya Watu Kitabibu,Lakini Polisi Anaokoa Maisha ya Madaktari kwa Kupambana na Majambazi nk.

Hili suala la "Kutukuza" Taaluma Fulani Nadhani ndio limepelekea Haya Yote. Sijaribu Kudharau Taaluma Yenu,inao Umuhimu wake kwa Nafasi yake Lakini hata Zingine zinao Umuhimu bila Walimu wa Shule ya Msingi Msingalikuwa hapa ,Wazungu husema "From Little Acorns a Oak Grows".

Mwalimu Nyerere aliwahi Zungumza "Wasomi ktk Nchi Maskini ni sawa na Wanakijiji wamejifunga,ili ukasome uje kuwatumikia,sasa ukishahitimu Elimu ile Unawakimbia kwenda Tafuta Maslahi Mazuri zaidi,Huu ni USALITI".

Hali duni ya Mishahara,Sekta ya Afya haitokani na Udhaifu wa kiutendaji wa hawa Mawaziri, bali uduni wa Kifedha wa Wizara na Serikali ikilinganishwa na Mahitaji ht Ukimuweka Ulimboka,Mkopi hamtafanya Miujiza, ktk Dunia ya tatu kote Sekta ya Afya ni Duni si kwetu tu,hii ni kuongopea Wananchi kwa Sababu mnazozijua ninyi.

Waziri Nkya,Waziri Mkuu walijaribu kuwaengage wakati wa Mgomo huo,mkawakwepa si mara moja Mama Nkya tulimuona, sote Tuliwaona. Sio serikali inayosababisha Watu wafe ni Ninyi ambao Mnaacha watu Wanakata Roho wakati uwezo na vifaa vya Kuwasaidia mnavyo na mmekuwa Mkivitumia Miaka yote leo mnasema hakuna jp ndio ni duni.

Hili Sisi Tutasahau Mwenyezi Mungu kamwe hatolisahau,Kutumia Uchungu wa Vifo vya Watanzania wenzenu Kama FIMBO YA KUILAZIMISHA SERIKALI KUTIMIZA MATAKWA YENU,kwenu ni Bora Binadamu afe kuliko Kukosa Maslahi,Mtizamo wa Ajabu sana kwa TRAINED DOCTOR. Mimi si Masihi naweza kuwa Wrong lakini hata Cardinal Pengo juzi alizungumzia Kuwa na "ROHO YA KIMUNGU" madaktari wale walioendelea kuhudumia Binadamu wenzao wakati wa Mgomo.

Namala najua Hutonipenda kwa Haya lakini Ukweli kama niuonavyo Lazima usemwe,Mnachofanya ni UKATILI USIOMITHILIKA Historia itawahukumu. Leo Mponda na Nkya Wajiuzulu,Kesho Wananchi Wakiandamana mfano Mkopi anyang'anywe Leseni ya Udaktari ana Kibri,Dharau na Katili? Serikali wakunyang'anye tu?
KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

No comments: