Tangazo

June 2, 2012

Mazoezi ya Taifa Stars jana jioni Leo wanakipiga na Ivory Coast


Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa, Kilimanjaro Taifa Stars wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast  leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Taifa Stars, Kim Poulsen akisimamia mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast

Mshambuliaji mahiri wa Kilimanjaro Taifa Stars, Mbwana Samatta akiweka saini kwenye madaftari ya vijana wa Ivory Coast mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast. Samatta amekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wengi wa Ivory Coast.

Kocha wa Makipa wa Kilimanjaro Taifa Stars, Juma Pondamali akiwanoa makipa wa timu hiyo ikiwa ni hatua ya mwiso kabla ya kuvaana na Ivory Coast kesho kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Taifa Stars, Kim Poulsen akizungumza na wachezaji wake mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kujiandaa na mechi  yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.

No comments: