Tangazo

June 15, 2012

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA MATIBABU YA FISTULA

Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akitoa maelezo wakati wa Uzinduzi  wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA Tanzania, uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar eSalaam Juni 15 2012, Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete. Mradi wa Fistula kwa mwaka inakadiriwa wastani wanawake wapya 2,500 hadi 3000 hupatwa na ugojwa huo wakati wanapojifungua. Kwa sasa wanawake zaidi ya 31,000 inasemekana wanalo tatizo la Fistula hapa nchini, Hivyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito wakina mama wenye matatizo ya Fistula kumuacha kujificha  kwani unatibika .hivyo waende katika matibabu ambayo hupatikana bure ktk  hosp. ya CCBRT jijini DSM na  hosp, ya Kilutheli ya Selian. (Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).   

Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, akiwa amemshika mtoto mchanga baada ya kukabidhiwa na wazazi wake baada ya ushuhuda walioutoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula- Tanzania. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT, Dk. Wilbroud Slaa.

Mke wa Rais NaMwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (mwenye miwani ) akiponyeza kitufe kuzindua kampeni hiyo.

Shuhuda wa ugonjwa wa FISTULA, Beatrice Mlunga (kulia) akitoa ushuhuda wa matatizo aliyoyapata ya ugojwa Fistula wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni mume wake,  Hosea Sanga.

Mama Kikwete akihutubia.

Mjomba Mpoto akiwatumbuiza waalikwa wakati wa Uzinduzi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na wasanii wa Kikundi cha Mrisho Mpoto pamoja na wafanyakazi wa CCBRT wakati wa uzinduzi.

Wasanii wa kikundi Mpoto wakifanya maigizo.


No comments: