Tangazo

June 19, 2012

RAIS AKUTANA NA WAZIRI WA HABARI NA UONGOZI WA RIADHA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (hayupo pichani) na viongozi wa chama cha riadha alipokutana nao kwa mazungumzo na kupanga mikakati ya namna ya kufufua mchezo wa riadha nchini. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Riadha nchini, William Kallaghe, Mkurugenzi wa Michezo. Bw. Leonard Thadei na (kushoto) ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha, Suleiman Nyambui.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini Dionis Malinzi baada ya kukutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na viongozi wa chama cha riadha alipokutana nao kwa mazungumzo na kupanga mikakati ya namna ya kufufua mchezo wa riadha nchini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Sethi Kamuhanda.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais wa Kamati ya Olimpiki Filbert Bayi baada ya kukutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na viongozi wa chama cha riadha alipokutana nao kwa mazungumzo na kupanga mikakati ya namna ya kufufua mchezo wa riadha nchini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Sethi Kamuhanda.

No comments: