Tangazo

September 4, 2012

Warembo 11 kuwania Taji la Redd’s Miss Kanda ya Kaskazini 2012

- Banana Zoro kutumbuiza
 
Na Mroki Mroki, Arusha

WAREMBO 11 wameingia kambini juzi Jijini Arusha kujifua kwaajili ya shindano la Redd’s Miss Kanda ya Kaskazini 2012, linalotaraji kufanyika jumamosi Septemba 8, 2012 jijini Arusha.

Warembo hao watapanda jukwaani katika Hoteli ya Naura Spring mjini humo kuwania taji hilo linalo shikiliwa na mrembo Stacy Alfred ambaye alinyakua taji la Mrembo mwenye Haiba ya Picha (Miss Photogenic 2011) katika Shindano la Miss Tanzania 2011.

Mwandaaji wa shindano hilo kupitia kampuni ya Jazz Promotions, Emma Mroso amesema kuwa maandalizi yote ya shindano hilo yanakwenda vyema na warembo wapo katika afya njema.

Aidha Mroso amewataja warembo walioingia kambini na wanaendelea na mazoezi yao kuwa ni Mishi Mziray, Dalina Hashim, Anita Mboya, Highmanna Lyimo, Anande Radhiel, Waridi Frenk, Buya Ernest, Lucy Stephano, Neyla Hashim, Trovina Mpanda na Theresia Kimolo.

Mratibu huyo amesema kuwa warembo hao walistaili kuwa 12 ikiwa ni warembo 3 kila mkoa kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga ispokuwa mshiriki mmoja Sara Benjamin anaumwa na yupo Nairobi kwa matibabu.

Shindano hilo linataraji kupambwa na burudani kali kutoka kwa Banan Zoro na kundi zima la B Band pamoja na wasanii wengine mbalimbali wa jijini Arusha.

Shindano la Redd’s Miss Kanda ya kaskazini 2012 limedhaminiwa na  Redd’s Original,  Dodoma Wine, Naura Springs Hotel,  Brazil Lounge,  Father kidevu Blog,  Modern holdings EA ltd, Honeys furniture, Little Roses, Jazz collection, Camro Insurance Services,   Eannaso,  Anyor Designs,   Triple A FM, Ndeku hair salon, Compumania celltronics,TLK investments, Computer and Secretarial College,  Arusha Art,  Cyber Net, Riverside Shuttle, eo security na Authentic Emergency Services.

No comments: