Tangazo

October 9, 2012

Redd's Miss Mbulu 2012 awa Miss Photogenic

Warembo walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo Genic.toka kulia ni Magdalena Roy (Mshiriki namba 6,kutoka Dar City Center - Kanda ya Ilala),Babylove Kalala (Mshiriki namba 9,kutoka Kagera - Kanda ya Ziwa),Lightness Michael (Mshiriki namba 5,kutoka Dodoma - Kanda ya Kati),Lucy Stephano (Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini) na Diana Hussein (Mshiriki namba 20,kutoka Dar Indian Ocean - Kanda ya Kinondoni.)

Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaaji Mkuu wa Mashindano ya Miss Tanzanzia,Hashim Lundega akitangaza Mshindi wa Redd's Miss Photo Genic ambaye ni Mshiriki kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano (katikati).hafla ya shindano hilo ilifanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa hoteli ya E'Manyata Lodge,Monduli jijini Arusha.



Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano ndie Redd's Miss Photo Genic 2012.Picha zote kwa hisani ya Intellectuals Communications Limited
************************
Na Mwandishi Wetu, Monduli
Redds MISS Mbulu Lucy Stephano juzi usiku alifanikiwa kukata tiketi ya kuingia 16 bora ya Redd’s Miss Tanzania, baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Redds Miss Photogenic.

Shindano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Emanyata Lodge, uliopo mjini hapa.

Lucy, alifanikiwa kuwashinda warembo wengine 30 wanaoshiriki Redds Miss Tanzania na kufanikiwa kutwaa taji hilo.

Mrembo huyo alifanikiwa kulitwaa taji hilo, baada ya ushindani mkali uliokuwepo kati yake na Redds Miss Dar Indian Ocean, Diana Hussein na Redds Miss Ilala namba mbili, Magdalena Roy.

Kutokana na kufanikiwa kwake kutwaa taji hilo, Lucy amefanikiwa kuvuka hatua moja kubwa zaidi ya kuliwania taji la Redds Miss Tanzania linalotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.

Mrembo mwingine anayetarajiwa kuingia hatua hiyo atapatikana Jumamosi katika ‘Usiku wa Redd’s Miss Tanzania’ mjini Arusha pale kutakapokuwa na kinyang’ayiro cha Miss Top Model.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments: