Tangazo

December 14, 2012

BLUE TOOTH SESSION NDANI YA CLUB BILICANAS KILA j’2

KATIKA kuhakikisha unatoa burudani kwa watu wa rika zote, ukumbi wenye hadhi ya kimataifa wa Club Bilicanas, jumapili hii utaanza kupiga disko maalum kwa watu wenye umri chini ya miaka 18 ‘Blue Tooth Session’ ambayo itakuwa ikifanyika ndani ya .

Mmoja ya viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omari amesema kwamba , lengo ni kuwapa burudani vijana hao ambao kutokana na umri wao hawawezi kupata fursa ya kuhudhuria burudani zinazofanyika usiku.

Amesema kuwa, pamoja na burudani ya muziki, vijana hao pia watapata fursa ya kushindana katika kusaka vipaji ambapo kiingilio kitakuwa sh 3,000.

Ameonngeza kuwa, kwa jioni mashabiki watapata burudani kutoka kwa wasanii wanaofanya vema katika muziki wa bongo fleva kupitia usiku wa 'Bongo Starz nite' ambapo kiingilio ni sh 6,000 kwa kila mmoja.

No comments: