Tangazo

March 6, 2013

Jaji Joseph Warioba kukutana na Waandishi wa Habari jijini Dar kesho Machi 07

Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba atakutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume, Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam, kesho (Alhamisi, Machi 7, 2013) kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Katika mkutano huo, Jaji Warioba atazungumzia uundwaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Waandishi wa Habari wa vyombo vyote mnakaribishwa.

Imetolewa na:
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania).

No comments: