Tangazo

March 13, 2013

Titanic Bar yaibuka Bingwa wa Nyama Choma

BAR ya Titanic ya Vingunguti, Jumapili Machi 10.2013, iliibuka kidedea katika fainali za Nyama Choma zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Safari Lager katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, hivyo kutwaa sh milioni moja.

Wakati Titanic ikijinyakulia kitita hicho nayo, Fyatanga ya Boko ilikamata nafasi ya pili na kubeba sh 800,000 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Assenga ya Buguruni iliyopata sh 600,000.

Aidha nafasi ya nne imekwenda kwa Soccer City ya Sinza iliyozoa sh 400,000 na Uhakiki Mbagala walioshika nafasi ya tano wakipata sh 200,000.

Akizungumzia vigezo vilivyotumika, Jaji Mkuu wa Safari Lager Nyama Choma, Doudlas Sakibu, alisema vilikuwa vingi, lakini kubwa zaidi ni kuangalia uandaaji nyama, mpaka hatua ya mwisho jinsi ya kupeleka kwa mteja.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hiyo, ameyataka makampuni mengine kuiga mfano wa Safari Lager na kuanzisha mashindano kwa lengo la kuongeza umoja na mshikamano kwa Watanzania.

Kwa upande wake Meneja wa Safari, Oscar Shelukindo, alisema shindano hilo litaendelea jijini Mwanza wiki hii na amewataka wadau mbalimbali jijini humo kukaa mkao wa kula.

No comments: