Tangazo

August 28, 2013

Washindi wa Airtel Yatosha Dar and Mwanza wakabidhiwa vitita vyao

Mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu, Bw. Nassoro Mohamed akiziangalia pesa taslimu shilingi milioni moja  alizokabidhiwa leo baada ya kuibuka mshindi katika promosheni hiyo. Bw. Nassoro ni mmoja kati ya washindi saba ambao wameweza kujishindia milioni moja kila mmoja kwa wiki hii kupitia promosheni hiyo. Kushoto kwake ni Happy Valence mmoja kati ya wafanyakazi wa Airtel baada ya kumkabidhi mshindi huyo kiasi hicho cha pesa.
Mmoja wa wafanyakazi wa Airtel, Jackline Kaaya akikabidhi shilingi milioni moja kwa Michael Joseph mkazi wa Mwanza, baada ya kuibuka mshindi kupitia promosheni maalumu ya Airtel inayofahamika kwa jina la Airtel yatosha shinda nyumba 3, inayowawezesha wateja wa Airtel  kote nchini kujishindia milioni moja kila siku. Tukio hilo fupi la kukabidhi zawadi hiyo lilifanyika katika ofisi za Airtel Mwanza.

No comments: