Tangazo

September 3, 2013

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA SADCOPAC

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizindua Kitabu cha Miaka 10  ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali   kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCOPAC) baada ya Kufungua Mkutano wa mwaka wa  WA SADCOPAC kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013. Kulia  kwake ni Spika wa Bunge Anne Makinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisindikizwa na  Spika wa Bunge, Anne Mkinda (kulia) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovic Utouh  baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka   wa  Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali   kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC) kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mzee wa Kimaasai akipuliza zumari wakati kikundi cha ngoma cha wamasai cha Arusha kilipotumbuiza katika mkutano wa mwaka wa  Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali   kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC) kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na washiriki wa  Mkutano wa Mwaka   wa  Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali   kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC)  baada ya kufungua  mkutano wao kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: